WAZIRI mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amesema suala la utapiamlo linatakiwa kuendelea kupigiwa kelele kwani bado ni kubwa hapa nchini na kusababisha udumavu kwa kiwango cha asilimia 31 kwa watu wake.
Pinda alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Nanenane kanda ya mashariki yanayoshirikisha mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga na Morogoro yanayoendelea viwanja vya Julius Nyerere.
Alisema suala la lishe bora ni vyema likapigiwa kelele na kuacha kubebeshwa lawama serikali kutokana na watoto wanaozaliwa nyakati nyingine kuwa na uzito mdogo.
Pinda alisema ya kwamba wataalamu wamekuwa wakieleza akinamama wajawazito wengi wamekuwa na upungufu wa damu na wanapofikia muda wa kujifungua na wanapata matatizo na hiyo kutokana na kula vyakula bila kujali lishe bora.
“Mimi natoka Katavi tunatamba kwa kulima mahindi lakini ugali wa mahindi niliozoea ni kwamba ukibolewa ulowekwe kwenye maji wiki moja halafu uanikwe kidogo na kupelekwa kusagwa mashine eti kupata ugali mzuri wa kunukia hii si hoja,”alisema Pinda
Alisema “Kumekuwa na mazoea kuwa wanaokula dona ni wafungwa pekee na hii si sawa pale watu wengi wanakula wanga (stach) ndani yake hakuna kitu sasa tuna mtihani mkubwa wa kusemea lishe,”alisisitiza Pinda
Alisema pamoja na mikoa ya Rukwa na Katavi kuongoza katika kulima zao la mahindi lakini mkoa hiyo ni miongoni mwa inayoongoza katika suala zima la utapiamlo.
Waziri mkuu Mstaafu alisema , wataalamu wamekuwa wakieleza kuwa ili kokomesha suala la utapiamlo ni lazima watu watumie mbogamboga ambacho ni chakula muhimu na kwamba ulimwengu unakili kuwa mboga zenye asili ya Afrika zimekuwa zikiongoza kwa lishe.
“Nataka tutoke hapa kwenda kulima bustani za mboga na sio kulima kwa ajili Biashara pekee bali kulima kwa kula ilikuweza kupata afya bora, hivyo nanenane kwangu tutumie kujifunza kilimo hicho,”alisema Pinda
Hivyo aliwataka wananchi kutumia ufugaji bora huku akiridhishwa na ufugaji bora hasa wa Samaki kwa kutumia njia za kisasa.
Pamoja na hayo alisema sekta ya kilimo bado ni muhimili kwa nchi hivyo kilimo kikiteteleka ni sawa na mtu akiteteleka na mgongo wake hivyo kilimo ni muhimu katika kuleta maendeleo.
Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kabla ya kumkaribisha Waziri mkuu Mstaafu Pinda, alisema katika kuondoa ukiritimba unaojitokeza ,wizara imeanzisha mfumo wa mazao ya Uvuvi, mifugo na mazao mengine (MIMIS) utakao wawezesha wadau wa mifugo wa zao ya uvuvi kufanya shughuli zao za kupata vibari na mambo mengine kwa haraka na urahisi.
Alisema wizara inaendelea kufanya mabadiliko katika mifumo mbalimbali ya kuoa urasimu na kuwataka wananchi kuondoka kwenye mifumo ya zamani , wizra inaendelea kuhamasisha wafugaji na wananchi kwa ujumla kuhusiana na chanjo mbalimbali za mifugo na sasa aina saba za chanjo zinazalishwa na kiwanda cha serikali.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro,Fatma Mwasa alisema kuwa mikoa inayounda Kanda hiyo imejipanga kuboresha maonesho ya Nanenane ili kuwezesha wananchi wajifunze teknolojia ya kilimo, mifugo na Uvuvi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa