1. Kuratibu usimamizi endelevu wa mazingira
2. Kuishauri Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika masuala ya usimamizi wa Mazingira.
3. Kuendeleza utunzaji na uhifadhi wa maliasili.
4 Kuandaa ripoti za mara kwa mara zinazohusu hali ya utunzaji wa mazingira.
5. Kukusanya na kusimamia taarifa za utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa maliasili katika Milima Uluguru.
6. Kufuatilia maandalizi, mapitio na uidhinishwaji wa uchambuzi wa athari za kimazingira zinazoweza kutokea kutokana na uwekezaji wa aina mbalimbali katika Jiji.
7. Kupitia sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa mazingira na za kisekta zinazohusu masuala ya mazingira.
8. Kuainisha na kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
9. Kutafiti maeneo mapya ya vivutio vya utalii katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
10. Kuandaa taarifa mbalimbali zinazohusu fursa za utalii katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
11. Kusimamia usafi wa Mji na Uzoaji wa Taka.
12. Kuhamasisha Kaya zifanye usafi katika mitaa yao kwa kuwatumia Bibi na Bwana Afya wa Kata
13. kusimamia mawakala wa usafi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa