Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema wakati awamu ya kwanza ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa Tanzania Bara inakwenda kukamilishwa mwezi Juni katika mkoa wa Dar-Es- Salaam kwenye uwanja wa Mkapa, awamu ya pili ya kampeni hiyo itaweka mkazo kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kuwa suala hilo limebainika kuwa ni uhitaji mkubwa kwa wananchi, na afisa ardhi yeyote atakaye bainika kuwa chanzo cha mgogoro wa ardhi p pote atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
"Katika ulimwengu huu wa teknolojia hatutegemei kuwepo na migogoro ya double allocation ya ardhi kwa kuwa shughuli zote zinafanyika kwenye mifumo, hivyo basi afisa ardhi anayesababisha migogoro kwa sababu ya kufanya double allocation, ni lazima tumchukulie hatua kali za kisheria ili kukomesha kabisa tatizo hili. Kufanya double allocation ya ardhi ni rushwa na ni lazima tupambane kuikomesha" alieleza Mhe. Ndumbaro.
Amesema awamu ya pili ya kampeni itafanyika kwenye maeneo yote ya awamu ya kwanza ili kubaini changamoto zilizokuwa zimesalia na kuzitatua zote kwa kuwa wizara itahakikisha miongoni mwa wanatimu wa kampeni ya awamu ya pili kunakuwa na mahakama tembezi (mobile court).
Aidha, Mhe. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuanzisha Kampeni hiyo ambayo imekuwa na manufaa sana kwa wananchi hasa wa maeneo ya pembezoni mwa nchi ambao mara nyingi hulazimika kusafiri umbali mrefu kufata huduma za msaada wa kisheria.
Amesema kampeni hiyo imekuwa mfano wa kuigwa kote ulimwenguni na imelifanya Taifa la Tanzania kuwa tajika ulimwenguni kote kwa kuwa ndio Taifa anzilishi la kampeni hiyo.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo alipokuwa akizungumza na Kamati Kuu ya Nanenane Kand ya Mashariki katika mkutano wa kamati hiyo uliofanyika tarehe 05.05.2025 kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maarufu kama uwanja wa nanenane mjini Morogoro.
Mkutano huo uliongozwa na mkuu wa mkowa wa Tanga, Mhe. Balozi Batilda Burhan na kuhudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Tanga, Pwani, Dar-es-salaam na Morogoro, wakuu wa wilaya za mikoa hiyo, wakurugenzi, wataalamu wa sekta husika.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa