WAKATI Tanzania (zamani Tanganyika) ikielekea kuadhimisha miaka 63 ya uhuru leo Disemba 9, 2024, Manispaa ya Morogoro imeiadhimisha siku hiyo kwa kuanza kufanya usafi katika Kituo cha Afya Mafiga na kupanda miti katika eneo hilo la Kituo cha Afya.
Tukio hilo la usafi na upandaji wa miti limefanyika Desemba 07-2024 huku mgeni rasmi akiwa Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho Mhe.Kihanga, amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendeleza utamaduni wa kupanda miti na kutoitelekeza miti iliyopandwa ili kutunza mazingira na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, Mhe. Kihanga, amesema kupanda miti ni muhimu katika utunzaji wa mazingira, kupata vivuli, hewa safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
" Tutakapokua na miti mingi katika Manispaa yetu ya Morogoro yetu itakua nzuri na mazingira yatakua mazuri hatutopata janga la njaa, upepo mkali wa kuezua majengo na hali nzuri ya hewa" Amesema Mhe. Kihanga.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba, amewataka wananchi wanaozunguka maeneo yaliyopandwa miti hiyo kuendelea kuitunza ila kuifanya Manispaa ya Morogoro kua na mazingira safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Naye Diwani wa Kata ya Mafiga,Mhe. Thomas Butabile, amewataka wananchi katika kuendelea kuenzi miaka 63 ya uhuru , wananchi waendelee kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka, upandaji wa miti na kuhakikisha wanashiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa ajili ya Maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa ujumla.
Katika maadhimisho hayo , watumishi pamoja na jamii kwa ujumla wameshiriki katika kufanya usafi maeneo yote ya Kata ya Mafiga husani katika kufyeka nyasi maeneo ya barabara , Ofisi za Serikali na taasisi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa