MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewatakaWatendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishwaji wa Mabomayote ya Shule ikiwemo Msingi na Sekondari ili wanafunzi waliofaulu waingiedarasani.
Kaulihiyo, ameitoa leo Desemba 21,2020 katika Shule ya Sekondari Kihonda ,wakati wa ziara ya kukagua Maboma yanayotakiwa kukamilishwa kwa ajili yakuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza waliofaulu.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Lukuba, amesema kuwa huu sio wakati wakuangalia pesa imeingia katika akaunti ya Kata au ya Shule kikubwa ni kasi yaujenzi iongezwe ili madarasa yakamilike kwa wakati na Wanafunzi wasome wakiwawamekaa katika madawati bila msongamano.
Lukuba,katika ziara hiyo amewasisitizia mafundi kwenda na kasi kubwa ili wanafunziwaanze kuyatumia madarasa hayo katika kupunguza msongamano darasani.
‘’ifikewakati sisi jamii ndio tuwe wa kwanza kuanzisha miradi kisha ndio serikaliiwekeze nguvu zake, nimekuja kuona maagizo ya Waziri Mkuu yanatekelezwaje, lakini nitoe rai kwa Watendaji wote wa Kata kwa kushirikianana , Watendaji wa Mitaa, kuwahimiza Wazazi na Wananchi kuongeza kasi yauhamasishaji katika kufanikisha ujenzi wa Maboma , agizo hili ni la Serikalitunatakiwa kulifanyia kazi kwa haraka, Baada ya tamko la Mhe. Rais la elimubure bila malipo Wazazi wamehamasika na kuwa na mwamko wa kusomeshaWatoto na Watoto wamefaulu hivyo ni wajibu wetu kuona Watoto hawa wotewaliofaulu ifikapo Januari 11/ 2021 wanaingia darasani , wanafunzi wetu wanauhaba wa madarasa hatutaki mrundikano, tunataka yakamilike wanafunzi wasomekatika mazingira ya kuachiana nafasi ili kuongeza kasi ya ufaulu, ukiwa katikamazingira mabaya hata ile hali ya ufundishaji inashuka, kazi nimeionainaendelea lakini ongezeni kasi tumalize kazi mapema" Amesema Lukuba.
Lukuba, amesema kuwa Jamii inaposhiriki ipasavyo kwa vitendo katika ujenzi wamiundo mbinu ya elimu huwa chachu ya kupata kilicho bora kabisa maana jamiihuwa na uchungu nacho kutokana kuwekeza nguvu zao na huwa walinziwakubwa.
Mwisho ametoa wito kwa wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro kuwa tayarikujitolea kwa hiari katika miradi ya maendeleo hususani katika Ujenzi wa Mabomaya Madarasa.
Shuleya Sekondari Kihonda ni miongoni mwa Shule iliyoingiziwa Shilingi Milioni 80,ambapo milioni 20 ni kwa ajili ya umaliziaji wa maboma 3 na shilingi milioni 60kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa mapya 3 kwani inategemea kupokea jumla yawanafunzi wa kidato cha kwanza 700.
Ikumbukwekuwa Jumla ya Wanafunzi waliofanya mtihani Darasa la saba ni 8401, Wasichana4336, Wavulana 4062 ambapo katika idadi hiyo jumla ya Wanafunzi 7577 walifaulumitihani miongoni mwao wasichana 3927, wavulana 3650 sawa na asilimia 90.22% yawanafunzi wote waliofaulu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa