1. MAHALI ULIPO:
Jengo hili la Ofisi ya Kata lipo Kata ya Mji Mkuu Mtaa wa Boma barabara iendayo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.
2. LENGO LA MRADI:
Kutoa huduma bora kwa Wananchi wa Kata ya Mjimkuu pamoja na Wananchi wengine wakazi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na kuongeza ufanisi wa kiutendaji watumishi wa ugani waliopo.
3.HATUA ZA UTEKELEZAJI:
Ujenzi wa Ofisi hii ulianza mwaka 2013 chini ya usimamizi wa Diwani wa Kata Hassan Maringo baada ya Wananchi kuibua ujenzi wa ofisi hii katika mchakato wa mpango shirikishi wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) ambapo matokeo ya Wananchi yalitoa kipaumbele cha ujenzi wa ofisi hii ya Kata.Mwaka 2016 jengo hili liliwekwa jiwe la msingi na mbio za Mwenge wa Uhuru.
4. GHARAMA ZA MRADI:
Hadi mradi huu kukamilika umegharimu kiasi cha Ths.64,237,665.00, fedha hizi zimetokana na vyanzo vifuatavyo:
JUMLA KUU … … … Tshs. 64,237,665.00
6. MANUFAA YA MRADI:
Kurahisisha utendaji wa kazi kwa Watumishi wa ugani pamoja na kuwa na mahali bora pa utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za serikali kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi na utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa