• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YATOA JUMLA YA MILIONI 517,800,000/= MIKOPO KWA VIKUNDI.

Posted on: June 17th, 2020

JUMLA ya shilingi milioni 517,800,000/=zimetolewa kwa ajili ya mikopo ya uwezeshaji kwa vikundi 72, ikihusisha vikundi 44 vya wanawake na vikundi 22 vya vijana pamoja na Vikundi 6 vya Watu wenye Ulemavu.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Sheria inayozitaka Halmashauri kutenga asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili mikopo ya uwezeshaji wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akikabidhi hundi za mikopo leoJuni 17, 2020 kwenye eneo la Shule ya Misingi Kiwanja cha Ndege kwa vikundi hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Regina Chonjo,amesema fedha walizokopeshwa zinapaswa kutumika kama chachu ya kuwaletea maendeleo.

Chonjo, amesema kuwa fedha walizokopeshwa wanapaswa kuzitumia katika malengo waliyoombea na siyo kupeleka katika matumizi mengine kama vile starehe na anasa ambazo zitawafanya washindwe kurejesha.

Aidha, amesema kuwa wanatakiwa kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vikundi vingine vya vijana , wanawake na walemavu waweze kukopeshwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na jamii inayowazunguka.

‘”Nawapongeza Wanavikudni wote kwa kukidhi vigezo vya kupewa mikopo na Manispaa ya Morogoro, Leo nimewakabidhi hundi hii ya mfano mbele ya waandiashi wa habari, ni imani yangu kuwa mtazitumia fedha hizi kwa malengo mliyojiwekea , hakikisheni mkopo huu unawanufaisha watu wote bila ubaguzi , naamini hakuna hata kikudni kimoja kitakachoniangusha , pia viongozi mliohudhuria hafla hii mtambue kuwa mmeingia mkataba wa kupewa mkopo kwa niaba ya Vikundi vyenu , hivyo mfanye shughuli ya pamoja kama mlivyoandika kwenye maandiko yenu ya mradi, lakini hatutaishia hapa bali tutafanya ufuatiliaji wa kukagua utekelezaji wa miradi yenu kuona maendeleo yenu” Amesema DC Chonjo.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya tano imekuwa pamoja sana na wananchi wanyonge hususani Wajasiriamali na inawapenda sana na inathamini mchango mkubwa unaoletwa na Wajasiriamali wadogowadogo katika kukuza pato la Taifa na ndio maana imeamua kutoa mkopo bila riba.

‘”Ni vye,ma mkajiuliza , ni wapi mtu unaweza kukopeshwa na kurejesha bila riba ?” Tuutendee haki mkopo huu na kurejesha kwa wkati ili kusaidia na wengine kupata fursa ya kukopo, tusimwangushe Rais wetu , yeye anatuonyesha kwa mfano : ni jasiri , mchapa kazi na anatekeleza kwa vitendo na kutoa matokeo makubwa bila woga, nasi hivyohivyo mkaitumie fursa hii ya mikopo mliyopewa kupata matokeo makubwa” Ameongeza DC Chonjo.

Wakati akikabidhi Bajaji 2 kwa vikundi hivyo, DC Chonjo, amesema wapo baadhi ya Viongozi ni wabinafsi na wanatabia ya kuweka maslahi yao mbele huku akisema wakati Serikali inapotaka kuwanunulia vikundi vifaa wao wanatafuta namna ya kuwarubuni ili wanunue wao ambapo jambo hilo amesema halikubaliki.

Amesema Serikali ya Rais John Pombe Magufuli siyo ya kununua vitu feki,vifaa vyote vipo kwenye viwango vinavyotakiwa , vyenye viwango bora ikiwa na lengo la kuhakikisha vinadumu kwa muda mrefu .

Pia amewaagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Maafisa Maendeleo ya Jamii wafuatilie na kusimamia mikopo iliyotolewa kwa vikundi kwani pesa hizo ni kodi za wananchi na ni lazima zirudishwe kwa wakati.

Mwisho ameendelea kuwasisitizia wananchi kuchukua hatua na kufuata taratibu zinazotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya ugonjwa wa CORONA hususani watu wanapokuwa katika shughuli za uzalishaji.

Kwa upande wa aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amesema kuwa mikopo waliyopewa haina riba kwa hiyo wanapaswa kurejesha fedha kulinga na kiwango walichopata.

Kihanga, amesema kuwa lengo la mikopo inayotolewa ni kuwakomboa vijana, wanawake na walemavu kutoka umaskini na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Nchi.

Amesema kuwa kikundi kitakachorejesha mkopo kwa wakati kitapewa mkopo mwingine zaidi ya ule walioupata awali.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema lengo la mfuko wa maendeleo ya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu ni kutoa fursa kwa jamii ili waweze kupata kwa urahisi mkopo usio na riba kwa wanavikundi kujidhamini wenyewe.

Lukuba amesema kuwa mikopo hiyo hutolewa ili kuongezea kujiendeleza kiuchumi na kuinua hali za maisha ili kuendena na kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ya kufikia uchumi wa kati.

“Kwa sasa Manispaa ya Morogoro imewapatia mikopo hii na nina imani kuwa mtaitumia mikopo hii vizuri kuboresha biashara zenu na kurejesha kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine viweze kukopa, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejenga imani na kufungua milango ya kuongezewa mikopo na hata kutoa fursa kwa wadau wengine wa maendeleo wanaojitokeza wenye nia ya kuwasaidia , wawasaidie kwa moyo” Amesema Lukuba.

Akitoa maelezo juu ya mikopo hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Bi Enedy Mwanakatwe , amesema katika kipindi cha mwezi huu Juni Manispaa ya Morogoro inatoa mkopo wenye thamani ya Shlingi Milioni 245,800,000.00 ambapo kiasi cha shilingi milioni 110,900,000.00 kwa vikundi 44 vya Wanawake na shilingi milioni 103,500,000.00 kwa vikundi vya Vijana na shilingi milioni 31,400,000.00 kwa vikundi 6 vya watu wenye ulemavu.

Mwanakatwe amesema kiasi cha shilingi milioni 272,000,000.00 tayari zimetengwa kwenye akaunti ya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu ambapo mchakato wa vikundi vitakavyopatiwa mkopo huo upo katika hatua za mwisho.

“Vikundi vinavyopewa mikopo ni vile ambavyo vimependekezwa na kamati ya maendeleo ya kata na kufanyiwa uhakiki na kuonekana kuwa vinakidhi vigezo, lakini pia tumevipa vipaumbele vikundi vinavyofanya shughuli za viwanda vidogodogo ambapo katika mkopo huu tumewanunulia Bajaji (3) na Mizinga ya nyuki 114” Amesema Mwanakatwe.

Hadi kufikia sasa Manispaa ya Morogoro imeshatoa milioni 517,800,000/= kwenye mwaka huu wa fedha 2019/2020 ikiwa ni mikopo ya vikundi mbalimbali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa