WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ,amewataka wafugaji nchini kuzalisha maziwa salama kwa afya Bora na uchumi endelevu.
Hayo ameyazungumza Juni 01-2025 katika kufunga maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ambapo uzinduzi wake ulifanyika Mei 27-2025.
Pia,amezitaka Taasisi binafsi za uzalishaji wa maziwa, waboreshe mnyororo wa uzalishaji mzima wa maziwa salama pamoja na kutengeza vipindi mahususi kwa ajili ya utangazaji wa kuhamasisha Watanzania kujua umuhimu wa kunywa maziwa salama.
Hata hivyo, Waziri Kijaji,amesema mpaka kufikia mwaka 2027, uzalishaji wa maziwa unatakiwa kufika lita 130 zinazohitajika kwa kunywa kwa Watanzania huku kila Halmashauri kuwe na mgahawa wa maziwa ili kila mtanzania anywe maziwa.
Waziri Kijaji,amesema katika kuona mifugo inakuwa salama,Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Juni 16-2025 anatarajia kuzindua chanjo na utambuzi wa mifugo.
Amesema chanjo hizo zina ruzuku kutoka Serikalini ambapo kwa upande wa Ng'ombe Serikali itachangia shilingi 500 na mfugaji atachangia shilingi 500 na upande wa kondoo na mbuzi Serikali itachangia shilingi 600 na mfugaji shilingi 600 hku chanjo kwa wafugaji wa kuku ni bure.
"Chanjo hizi za mifugo tayari Dkt Samia kashatupa maelekezo, na tayari dozi za zaidi ya milioni 19 za Ng'ombe zimeshambazwa Halmashauri zote nchini na dozi zaidi ya milioni 17 za mbuzi na kondoo nazo zimesambazwa, nitoe wito wafugaji mkachanje mifugo yenu kwa wakati ili kuendelea kuwa na mifugo bora itakayoweza kuzalisha maziwa salama kwa viwango vikubwa.
Kuhusu utambuzi wa mifugo,Dkt.Kijaji amesema kuwa Serikali ishatengeneza hereni zaidi ya milioni 36 za Kijidigitali kwa ajili ya utambuzi wa mifugo ili kuweza kukidhi matakwa ya soko la ufugaji.
Amesema kuwa utambuzi huo wa mifugo, utasaidia kudhibiti uwizi wa mifugo na kusaidia udhibiti wa upotevu wa mifugo kwa wafugaji.
Katika kuboresha huduma za wafugaji , amesema Serikali imeshanunua zaidi ya pikipiki 700 kwa ajili ya maafisa ugani ili waweze kuwafikia wafugaji kwa urahisi na kuwapa elimu bora ya ufugaji.
Aidha, Dkt.Kijaji , amewataka wafanyabiashara ya mifugo nchini hususani wanaosafirisha mifugo hiyo kwenda nje ya nchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi kwani katika uongozi wake hatakubali kuona utoroshaji wa mifugo kwenye minada unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, amemshukuru waziri Kijaji kwa kuuteua Mkoa wa Morogoro kuwa mkoa wa Mbadiliko ya Sekta ya Mifugo nchini.
RC Malima, amesema kuwa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye mifugo mingi ambayo sifa yake kubwa ni kusababisha migogoro hivyo inatakiwa kubadilishwa mtazamo.
Aidha,RC Maliama,amesema tija ya uzalishaji wa maziwa ni ndogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya teknolojia duni za ufugaji Elimu zaidi itolewe kwa wafugaji ili wafuge kisasa.
Hata hvyo,RC Malima, ameiomba Wizara ya Mifugo kuuboreshea nyama, maziwa kwa kuongeza ubora wa Ng'ombe na uzalishaji wa maziwa salama kwa watumiaji.
Pia,RC Malima ,amemuomba Waziri wa Mifugo wafugaji wa Mkoa wa Morogoro waongezewe akiba ya visima vya maji safi na salama kwenye miji ya wafugaji ili upande wa Kilosa wapate visima 10 na Mvomero 10 kuepusha mifugo kutembea umbali mrefu kutafuta maji ili yale maji na majani wakila mifugo wataongeza uzalishaji wa maziwa.
Kuhusu vyama vya ushirika, RC Malima ,amesema tayari mkakati wa kuviombea mikopo vyma hivyo umeshaanza ili kuendelea kuvipa nguvu na kuleta mabadiliko makubwa kama ilivyokusidiwa na Wizara ya Mifugo kupitia vyama hivyo.
Naye Msajili wa Bodi ya Maziwani Nchini. Prof. George Msalya, amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kufungua fursa za kwenje tasnia ya maziwa kwa kutambua kuwa maziwa ni lishe na uchumi.
"Maziwa yanayozalishwa hapa nchini yanachangia Kwa asilimia mbili kwenye pato la Taifa huku tasnia hiyo ya maziwa ikikua kwa asilimia 2.3,"Amesema Prof. Msalya.
Katika ufungaji wa maadhimisho hayo ya Maziwa Kitaifa, zawadi mbalimbali zilitolewa kwa baadhi ya Taasisi/wadau mbalimbali waliofanya vizuri katika tasnia ya uzalishaji wa maziwa.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mwaka 2025 " Maziwa Salama Kwa afya Bora na Uchumi Endelevu".
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa