• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA MOROGORO MJINI AFURAHISHWA NA UTULIVU WA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

Posted on: February 3rd, 2020

Afisa Mwandikishaji jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, amefurahishwa na utulivu unaoendelea katika zoezi zima la Uboreshaji Daftari la Kudumu la wapiga kura lililoanza leo Februari 3 hadi 9 mwaka huu 2020 katika Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Sheilla , amesema utulivu unaoendelea ni kiashiria tosha cha kwamba zoezi hilo litamalizika vizuri.

Amesema kuchaguliwa kwao kumetokana na kuaminiwa na hivyo wanapaswa kutambua uzito na umuhimu wa zoezi hilo na kuwataka watekeleze zoezi hilo kikamilifu.

Aidha,amechukua nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutekeleza haki zao za msingi za kikatiba na hatimaye kwenda kuwachagua Viongozi watakao weza kuwaletea maendeleo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa Diwani, Mbunge na Rais.

Aidha amesema kuwa katika  zoezi hilo, wataandikishwa wapiga kura wapya, kwa maana ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha mwaka 2015, ambao wametimiza miaka 18 au watakao kuwa na umri wa miaka 18 ifikapo 2020, pia watapatiwa vitambulisho vipya kwa waliopoteza au kuharibika vitambulisho vya awali na watafutwa kwenye Daftari wale ambao wamepoteza sifa za kuwa wapiga Kura.

"Kikubwa ninachowaomba Waandikishaji kwamba wakati zoezi hili likiendelea hakikisheni mnakuwa  karibu na wananchi wakati wa zoezi hili ili kumfanya aweze kutoa taarifa zilizosahihi za mpiga Kura na kuziingiza katika mfumo." Amesema Sheilla.

Katika hatua nyingine, amewataka Wenyeviti wa Mitaa,  Maafisa Watendaji wa Mitaa na Kata pamoja na Wananchi kwa ujumla kuhamasishana ili watu wote wenye sifa waweze kuandikishwa na kupata haki zao za kikatiba katika kushiriki chaguzi zijazo.

Naye,  Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo,amewataka waandikishaji hao kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kutekeleza zoezi hilo kwa  kwa umakini na ufanisi pamoja na  utunzaji wa vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.

Amesema matarajio yake ni kuona  zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura linafanikiwa kwa kiwango kikubwa ili kuwa na taarifa sahihi za wapiga Kura.

Pia amesisitizia umuhimu wa kuzingatia umakini katika maeneo yao ya kazi ikiwemo usambazaji wa vifaa na ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa wakati uliopangwa.

Hata hivyo amewaambia wasisite kuwasiliana na Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao.

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Afisa mwandikishaji Jimbo la Morogoro imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na hivyo nanyi mna kazi ya kuhakikisha kuwa mnatekeleza kikamilifu kwa upande wenu" amesema Kombo.

Mwisho amewataka waandikishaji kutekeleza majukumu yao waliyopewa kwa umakini, uaminifu, uadilifu na uweledi wa hali ya juu.

Kwa upande wa Mwananchi, Shafii Juma Fundi, amesema zoezi hilo ni zuri huku akiwasihi  wananchi wenzake kujitokeza kwa wingi ili kupunguza usumbufu wakati zoezi hilo litakapoelekea mwishoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa