Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na Wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Morogoro wamekutana kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kukumbushwa kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia na ujazaji kamili wa wadhamini kuelekea uandikishaji wa Wapiga kura utakaofanyika tarehe 11-20 mwezi Oktoba 2024.
Akizungumza kwenye kikao hiko Oktoba 08-2024 , Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi kwa niaba ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba, amesema lengo la kikao hiko ni kuwakumbusha vyama vya siasa kuwa wanao wajibu na haki ya kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia wapiga kura Pamoja na kuwahamasisha wanachama wao kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
“Tarehe 11-20 Oktoba 2024 tunakwenda kuanza uandikishaji wa wapiga kura,ni vema sasa tumeona tuwashirikishe wadau na viongozi wa vyama vya siasa vyote ili kuhamasisha wanachama na wafuasi wenu waweze kujiandikisha , tumeitana ili kukumbushana mambo muhimu ili uchaguzi wetu uwe huru naa wa haki " Amesema Komba .
Naye Afisa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Shabani Duru,amesema vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni
Duru amesema zoezi la kujiandikisha llitaanza tarehe 11-20 mwezi Oktoba hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa