• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

ANWANI ZA MAKAZI KUIBADILISHA TANZANIA KUWA YA KIDIJITALI

Posted on: January 14th, 2022

SERIKALI imejikita kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi nchi nzima kwa lengo la kuibadilisha Tanzania kuwa ya kidijitali kwa kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi wa kila mwananchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye amewakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonaz wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wataalam wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi.

Dkt. Yonazi amesema kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi ili kila mwananchi aweze kutambuliwa pale alipo ambapo nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mtaa, barabara, inakuwa na jina la mtaa na kila nyumba inakuwa na namba ya nyumba

Vile vile, ameitaka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kusimamia utekelezaji wa mfumo huu ili ifikapo Mwezi Mei mwaka huu jambo hili liwe limekamilika kwa kuwa utekelezaji wa mfumo huu utaiwezesha Serikali kuwa na sensa bora ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inayoratibu jambo hili, imeelekeza taasisi zote za Serikali nchi nzima zinatekeleza mfumo huu wamiliki wote wa majengo na nyumba nao waweke namba za nyumba kwenye nyumba na majengo yao na wataalam wote waliojengewa uwezo watumike vizuri kutekeleza mfumo wa anwani za makazi na postikodi na jambo hili liwe ajenda kwenye vikao

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela amesema kuwa kimsingi tumechelewa kutekeleza mfumo huu wa anwani za makazi, ila kwa kuwa viongozi mtajengewa uelewa, ni matumaini yangu kuwa kwa pamoja tutashirikiana na wataalam wetu kutekeleza jambo hili kwenye maeneo yetu ndani ya muda uliopangwa na niahidi kuwa Mkoa wa Morogoro hatutawaangusha Wizara.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi na postikodi ni moja ya aina ya mawasiliano kama zilivyo aina nyingine za mawasiliano na mfumo huu unahusisha eneo husika ambapo utamuwezesha mwananchi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine; utarahisisha shughuli za kiuchumi, kijamii na utawala.

Mhandisi Ichwekeleza ,ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kufanya vizuri katika zoezi la mfano la uandikishaji wa anwani za Makazi.

Wakitoa salamu za shukrani kwa niaba ya viongozi wengine, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma, amesema kuwa viongozi watoe majina ya mitaa ndani ya siku moja ili kufanikisha utekelezaji.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema watahamasisha wananchi kununua vibao vya nyumba ili kufanikisha uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi ndani ya Mkoa.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya zoezi la uandikishwaji wa anwani za Makazi kukamilika basi anwani hiyo itakuwa ni msingi wa Utambuzi wa Kila Mwananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa