Baraza la Maendeleo Kata ya Mafiga, limewezesha kaya 100 za wazee kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa ambapo malengo yao ni kuona wazee wanaendelea kupata huduma za afya bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kadi hizo zimetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kata ya Mafiga eneo la Kituo cha Afya Mafiga.
Akizungumza mara baada ya mgeni rasmi kukabidhi kadi hizo, Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kutimiza ahadi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Tumetoa Bima hizi kwa kaya 100 mpaka sasa lakini kaka yangu Mhe. Chomoka amenihakikishia kadi 100 nyingine hii ni hatua kubwa na kuona sasa tunakwenda kuhakikisha wazee wetu wanapata huduma ya Afya kwa uhakika mwaka mzima” Amesema Butabile.
Mwisho, Mhe. Butabile amewataka wananchi wa Kata ya Mafiga kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii.
Kwa upande wa Wazee ambao ni wanufaika wameshukuru jitihada za Diwani na Baraza lake la Maendeleo kwa kuwawezesha kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya huku wakiwasii viongozi wengine kuiga mfano huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa