• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO AMCHARUKIA MKANDARASI UJENZI WA SOKO MANISPAA YA MOROGORO.

Posted on: April 16th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amemtaka Mkandarasi wa Soko Kuu la Kisasa kufanyakazi kwa ushirikiano na mkandarasi aliyeteuliwa kujenga paa la jengo la soko hilo ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.


Hayo ameyasema leo, Aprili 16, 2020 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwemo mradi wa Soko pamoja na Stendi ya Daladala.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema mradi huo umekaa muda mrefu sana , hivyo mkandarasi lazima aonyeshe ushirikiano na moyo wa kizalendo katika kutumia fedha za kodi za Wananchi ambazo Mhe. Rais, Dtk. John Magufuli amezitafuta kwa tabu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.


Aidha, amemtaka Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa,, kuwa mzalendo na kukamilisha mradi huo kwa wakati.


”Muwe wazalendo, mlituambia kwamba mtatuwekea Paa la Soko kwa gharama nafuu, cha ajabu kwamba mkatuambia Bilioni 1.2 , sasa tumeamua kutafuta mzawa mwenye mapenzi mema akatupunguzia hadi kufikia Milioni 859 na VAT juu, nyie mnawakatalia kuingia Sokoni na kutowapa ushirikiano, ni kitu cha ajabu sana mkiambiwa nyie ndio mnaokwamisha mradi tutakuwa tunawaonea? Mhe. Waziri Jaffo akisikia hii unafikiri itakuwaje? Tuwe wazalendo mradi huu ni wa wananchi , kule tumewapanga kwa muda tunatarajia mradi huu ukamilike ili tuwarudishe hapa na nyinyi mnatukwamisha, shirikianeni mkifanya kazi nzuri ndio mnazidi kujitangaza” Ameongeza DC Chonjo.

Amesema katika ziara ya Mkuu wa Mkoa , walikubaliana kuangalia kiasi nafuu cha kuweka paa la Soko lakini cha kushangaza bei waliyokuja nayo ni kubwa huku akijua kwamba Manispaa hiyo haina uwezo wa kununua.



”Muwe wazalendo, mlituambia kwamba mtatufanyia kwa gharama nafuu, cha ajabu kwamba mkatuambia Bilioni 1.2 , sasa tumeamua kutafuta mzawa mwenye mapenzi mema akatupunguzia hadi kufikia Milioni 859 nna VAT juu mnawakatalia kuingia Sokoni na kutowapa ushirikiano, ni kitu cha ajabu sana mkiambiwa nyie ndio mnaokwamisha mradi tutakuwa tunawaonea? Mhe. Waziri Jaffo akisikia hii unafikiri itakuwaje? Tuwe wazalendo mradi huu ni wa wananchi , kule tumewapanga kwa muda tunatarajia mradi huu ukamilike ili tuwarudishe hapa na nyinyi mnatukwamisha, shirikianeni mkifanya kazi nzuri ndio mnazidi kujitangaza” Amesema DC Chonjo.


"Ujenzi huu wa mradi wa Soko ulipaswa kumalizika tarehe 31, Desemba, 2019 lakini kutokana na ukiritimba wake mradi ukachelewa , alishatuambia hawezi kuweka paa kwa bei ndogo, tukatafuta mtu ambaye ataendana na bei zetu tukampata lakini bado akaendelea kumuwekea vikwazo badala ya kushirikiana na wenzake, kwa maana hiyo inaonekana kuwa yeye ndio kikwazo cha kukwamisha mradi huu, katika vikao vyote vya mchakato wa kumpata mtu wa bei nafuu wa kuezeka paa la Soko alishirikishwa leo anakuja kutukwamisha hatuwezi kuvumilia , tunachokiomba waendelee kushirikiana ili mradi huu umalizike kwa wakati"Ameongeza Chonjo.


Amesema Wafanyabiashara wametengewa maeneo kwa muda, lakini wanapokwenda kuwaambia wasipange biashara chini wanaleta chuki na Serikali yao , hivyo lazima Soko hilo likamilike kwa wakati na kuwaondolea adha wafanyabiashara.


Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro imekuwa wazalendo sana kwani imemvumilia sana Mkandarasi hivyo wao wanatakiwa kuheshimu maamuzi yao kwa kufanya kazi na kukamilisha mradi kwa wakati.

Amesema miradi hiyo inasubiriwa na Wananchi , kwahiyo kukamilika kwa miradi ita pelekea kuanza kutoa huduma bora kwa Wananchi na kuongeza mapato kwa Halmashauri.


Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim, amesema wameyapokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya hivyo watajitahidi kukaa na Wakandarasi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.

Naye Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, amesema mradi  wa Stendi ya Daladala umefikia asilimia 90, ambapo Jengo la Utawala ni asilimia 95 na Jengo la Ulinzi asilimia 92% hivyo hadi kufikia tarehe 25, mwezi Mei, 2020 mradi huo utakuwa umekamilika licha ya kuwepo kwa changamoto kama vile mvua na uwepo wa ugonjwa wa CORONA.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa