• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO ATOA MASAA 24 KWA MAAFISA TARAFA KUTOA TAARIFA KAMILI ZA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WILAYA YA MOROGORO

Posted on: February 19th, 2020

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amewataka Maafisa Tarafa wa Wilaya ya Morogoro kutoa taarifa na takwimu halisi  ndani ya masaa 24 kuhusu vitambulisho walivyokabidhiwa vya Wajasiriamali na taarifa zifikishwe kwa Katibu Tawala wa Wilaya kesho Tarehe 20 , 2020 saa 2:00 Asubuhi .

Hayo ameyasema leo Februari 19,2020 Ofisini Kwake  kufuatia kikao alichokiitisha dhidi ya Maafisa Tarafa juu ya utoaji wa taarifa ya ugawaji wa Vitambulisho kwa Wafanyabiashara wadogowadogo Wilaya ya Morogoro hadi kufikia tarehe 14,Februali 2020.

Aidha ametoa taarifa na takwimu kwa Tarafa zilizokabidhiwa Vitambulisho hivyo ambapo jumla ya Tarafa saba zilizopo ndani ya Wilaya ya Morogoro zilikabidhiwa Vitambulisho hivyo kufuatia kauli iliyotolewa na Serikali kwamba Wakuu wa Wilaya wawakabidhi zoezi hilo Wakurugenzi wa Manispaa.

Amesema taarifa zinazotakiwa kuwasilishwa katika Ofisi yake  ni pamoja na vitambulisho vilivyokabidhiwa Wilayani, Vitambulisho vilivyokabidhiwa katika Tarafa, Vitambulisho vilivyouzwa vikionesha thamani ya pesa, Vitambulisho fedha zake zilizopelekwa benki, fedha ambazo hazijapelekwa benki pamoja na Vitambulisho vilivyobakia.

Katika taarifa aliyoisoma kupitia tarafa zote 7  za Wilaya ya Morogoro, zimeonesha kuwa Tarafa ya Manispaa ilikabidhiwa vitambulisho 13,146 vyenye thamani ya Tshs 262,920,000.00 na kuuza vitambulisho vyote ambapo jumla yake ni Tshs 262,920,000.00 sawa na asilimia 100, Tarafa ya Mikese walipewa vitambulisho 900 thamani ya Tshs 18,000,000.00 na kuuza 853 kwa shilingi 17,060,000.00 sawa na asilimia 94.78 na kubakiza 37, Tarafa ya Mvuha walipewa vitambulisho 570 vyenye thamani ya tshs 13,000,000.00 na kubakiza 71, Tarafa ya Bwakila vitambulisho 830 na kuuza 772 vilivyobaki ni 34, Tarafa ya Ngerengere walipewa vitambulisho 998, kuuza 903 na vilivyobaki 90, Tarafa ya Mkuyuni vitambulisho 1100, waliuza 822 na kubakia 278 pamoja na Tarafa ya Matombo ambao walipewa vitambulisho 950, kuuza 788 na kubakia na 147.

Aidha, amesema katika Wilaya ya Morogoro, Vitambulisho vya Wajasiriamali wadogowadogo vilivyokabidhiwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mwaka  2019 vilikuwa   18,500 ambapo awali zoezi hilo lilikuwa likisimamiwa  na Wakuu wa Wilaya kabla ya kulishusha kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa.

Katika hatua nyingine, amewataka Maafisa Tarafa wahakikishe ifikapo kesho Saa 2:00 asubuhi taarifa zote za Vitambulisho vya Wajasiriamali ziwe zimewasilishwa kwa Katibu Tawala wa Wilaya ili aweze kuzikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Olata Sanare kwa mujibu wa maelekezo waliyopatiwa.

"Tusifanye mchezo , nataka kesho mapema muanze leo kuwasumbua hao watendaji wenu taarifa hizi tulishatoa na mwisho ni kesho Februali 20,2020 pamoja na kutoa muda mrefu  mkaona kama utani sasa kesho nazitaka na pesa hizi za Mhe. Rais Dkt John Magufuli haziliwi na kama wapo waliozila watazitapika adhabu yake ni Mahakamani na hakuna dhamana zaidi ya kurudisha pesa hizo, mmepewa dhamana nataka kazi hiyo ifanyike leo hii mpaka saa 12 jioni muwenazo taarifa zote "Amesema DC Chonjo.

Hata hivyo amewataka Maafisa Tarafa kufanya kazi kwa kutambua majukumu yao na nguvu waliyonayo ili kuwaletea Wananchi maendeleo ikiwemo kutatua kero za wananchi kwa kupanga vipaumbele vyao katika maeneo wanayoishi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa