Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo amewataka wafanyabiashara waliondolewa kufanya biashara zao maeneo ya mjini kati kuhakikisha wanarudi maeneo ya masoko waliyopangiwa na atakaekiuka atashukuliwa hatua kali za kisheria.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake kufuatia kufanyika zoezi maaalumu la kuwaondoa wafanyabaishara waliokuwa wamezagaa maeneo ya mjini kati kuuza bidhaa zao katika sehemu ambazo sio rasmi .
Alisema kuwa kufuatia wafanyabiashara kuzagaaa maeneo ya mjini kati na kufanya biashara sehemu zisizo rasmi huku maeneo ya masoko yakiachwa wazi ilipelekea Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuendesha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashra hao ili waweze kurudi maeneo waliyopangiwa.
Alisema kuwa kutokana na wafanyabaishara hao kutofanya biashara katika maeneo rasmi inaipelekea Halmashauri kukosa mapato,kuweka mji katika hali ya uchafu,kuziba kwa mitaro ya maji ya mvua kwa kutupa takakataka hovyo.
‘’Pia wafanyabaishara hao wanapozagaa kiholela inaleta adha kwa watembea kwa miguu na wenye magari na pia ni rahisi kuwepo kwa mlipuko wa magonjwa kutokea ama kuenea maeneo mengi kwa haraka’’alisema Chonjo.
Aidha aliwataka wafanyabiashara walioondolea kuyatumia masoko yaliyopo ikiwemo soko la Chamwino,Manzese,Mwembesongo ,Madizini ,Kihonda Magorofani na Kichangani ambayo yameachwa wazi na badala yake wafanyabiashara kukimbilia maeneo ya mjini kati.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa onyo kwa wafanyabishara na wanunuzi wa bidhaa watakaobainika kufanya shughuli hizo mjini ikiwemo kununua watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupandishwwa mahakamani.
Nae mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro Habiba Thabit aliipongeza serikali ya wilaya kwa kushirikiana na halmashauri kuwaondoa wafanyabiashara hao wavamizi kwani walikuwa wanawapa shida watembea kwa miguu kutokana na bidhaa zao kupangwa barabani na hivyo kuhofia kugongwa na magari.
Pia Mkaguzi kutoka Wakala wa barabara TANROAD Mkoani Morogoro Benjamin Mwendapole alisema kuwa mfanyabiashara yoyote atakebainika kuuza bidhaa zake nje ya duka atachukuliwa hatua kali za kisheria lengo ni kuhakikisha kila mfanyabiashara anafanya biashara katika eneo lake bila kumbughudhi mtu mwingine ama kumzuia mwenda kwa miguu kupita.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa