• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC MSANDO AZINDUA MIONGOZO YA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO, AITAKA MANISPAA KUJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIELIMU

Posted on: September 29th, 2022

MKUU wa wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amezindua miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa elimu Manispaa ya Morogoro huku akiitaka Manispaa kujikita na changamoto za ndani zaidi katika eneo la elimu.

Kauli hiyo ,ameitoa Septemba 29/2022 alipokuwa akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi na Sekondari na viongozi wa Manispaa ya Morogoro kwenye uzinduzi wa miongozo hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilakala.

DC Msando, amesema Manispaa ya Morogoro , hakuna sababu ya kutofanya vizuri katika suala la kitaaluma kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia ikilinganisha na Halmashauri nyingine katika mkoa wa Morogoro.

Aidha, amesema kuwa , miongozo hiyo hususani wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu ya msingi ni mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji,usimamizi na ufuatiliaji na ushiriki wa wadau ili kufanikisha utekelezaji huo.

Hivyo,amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari kutumia miongozo ya usimamizi na uendeshaji iliyotolewa na serikali kufanya tathimini ya mara kwa mara ya hali ya elimu ili kurudisha heshima ya Manispaa ya Morogoro.


Ametoa agizo kuanza kuwafuatilia na kuwaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza elimu ya awali na shule ya msingi ili waanze masomo ifikapo mwezi Januari 2023 na kusimamia watoto watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wawe wameripoti mara shule zitakapofunguliwa.

Miongozo iliyozinduliwa katika Halmashauri hiyo,ni mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu ya msingi,uteuzi wa viongozi wa elimu katika mamlaka za serikali za mitaa na changamoto katika uboreshaji wa elimu ya msingi na sekondari.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewahimiza walimu kuwa wabunifu, kujifunza ikiwamo kusoma vitabu mara kwa mara ili kupata maarifa na mbinu mpya zitakazowasaidia kufanya vizuri katika kazi zao za kila siku.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Chausiku Masegenya, alisema wamejipanga kufanya vizuri katika sekta ya elimu ili watoto wote waliopo kwenye shule za msingi na sekondari wapate elimu bora na hatimaye waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Naye Afisa elimu sekondari Manispaa ya Morogoro, Gabriel Paul, amesema Manispaa ya Morogoro ina Shule za Sekondari za Serikali 27 na binafsi 28 na kueleza uzinduzi wa miongozo utasaidia katika ufundishaji na kukabiliana na changamoto mbalimbali .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa