• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAIPONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Posted on: September 23rd, 2021

HALMASHAURI ya mji Kibaha imetoa pongezi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wananchi wa Manispaa hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa Septemba 23, 2021 wakati wa ziara ya kamati ya fedha ya Halmashauri ya Mji Kibaha ndani ya Manispaa hiyo kwa ajili ya kujifunza miradi mikubwa ya maendelea ikiwemo Soko kuu la Chifu Kingalu na stendi ya Mabasi ya Msamvu.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe. Mussa Ndomba amesema kuwa kitendo cha Manispaa ya Morogoro kutekeleza miradi ya maendeleo ni moja ya hatua kubwa ya kuhakikisha ya kwamba wananchi wanapata huduma bora

“Tunawapongeza sana Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza miradi hii mikubwa ya maendeleo, soko kuu pamoja na kituo cha mabasi cha kisasa Msamvu ni hatua kubwa mno mmeifanya, tumeona mmefanikiwa jinsi ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo wadogo, sisi tumekuja kujifunza kutoka kwenu na tunakwenda kutekeleza katika Halmashauri yetu.” Amesema Mhe. Mussa.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema kwa mwaka Manispaa ya Morogoro inakusanya zadi ya Bilioni 11 , hivyo kuongezeka kwa vitega uchumi vitasaidia kuongeza Zaidi pato la Manispaa.

“Sisi tumewatangulia, tunaamini kujifunza kwenu hapa, mnaweza nyinyi mkafanya vizuri Zaidi yetu sisi, Manispaa yetu ni chuo cha kujifunzia kwahiyo ujio wenu kwetu unatufanya na sisi tuongeze nguvu katika kutafuta vyanzo vyengine vya mapato” Amesema Mhe. Kihanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha,Msham Mbunde,ameongeza kuwa Manispaa ya Morogoro ina vitega uchumi vingi na kutokana na kujifunza vitega uchumi hivyo wanaweza kufanya vizuri Zaidi yao.

“Naamini kwa kutupokea huku na kukubali tupitie vitega uchumi vyenu ili tuone wenzetu mmefanya vitu gani kwani kimapato mpo juu, tunawapongeza sana na tumeona mmestahili kuwa Manispaa na naamini kwa kijifunza huku tunaweza kufanya vizuri zaidi yenu.” Amesema Mbunde.

Aidha kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,Michael Waluse, amesema kuwa uamuzi walioufanya wa kujenga kituo cha kisasa cha mabasi Msamvu ni chanzo kikubwa cha mapato kwenye Halmashauri

“Tumeamua kujenga Kituo cha kisasa na ni chanzo kikubwa cha mapato kwenye Halmashauri yetu, hivyo Halmashauri ina mpango wa kufunga mitambo ya kisasa ya kukusanya mapato kwa sababu hili ni eneo ambalo linahitaji ufatiliaji wa karibu sana, ndio maana tutafunga mitambo ya kisasa.” Amesema Waluse.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa