• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

KAMATI YA USHAURI WILAYA YAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI YENYE JUMLA YA TSH 75,372,267,796.32 KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021.

Posted on: February 7th, 2020

Kamati ya Ushauri Wilaya imeridhia na kupitisha jumla ya Tsh 75,372,267,796.32 ikiwa ni mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 ikijumuisha mapato ya Ruzuku na mapato ya ndani.

Hayo yamebainishwa na Mchumi wa Manispaa Sadoth Kaijage wakati akiwasilisha bajeti ya Halmashauri katika kikao cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika leo Februari 7 katika ukumbi wa mikutano.

Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inakisia kukusanya kiasi cha Tshs 8,478,799,224.32 ambapo Tsh 498,870,893.41 ni uchangiaji wa huduma za afya na Tshs 271,759,000.00 ni uchangiaji wa ada za wanafunzi kutoka katika vyanzo vya ndani na kiasi hicho ni ongezeko la Tsh 1,772,873,011.45 ambayo ni sawa na asilimia 26.43 ya makadirio ya mwaka 2019/2020 ya Tshs 6,705,926,212.87.

Aidha katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inatarajia kupokea  kiasi cha Tsh 7,483,018,572 kutoka Serikali kuu na wahisani mbalimbali kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo Serikali kuu wanatarajia kuchangia kiasi cha Tsh 5,832,810,000 na Tsh 1,650,208,572 ikiwa ni fedha za nje.

Pia ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inatarajia kutumia kiasi cha Tsh 59,410,450,000.00 kutoka Serikali kuu kwaajili ya matumizi ya kawaida ya mishahara na matumizi mengineyo ambapo matumizi kwaajili ya matumizi mengineyo yanakisiwa kuwa Tsh 2,495,867,000.00 na itapokea kiasi cha Tsh 2,495,867,000.00 ikiwa ni ruzuku ya matumizi ya kawaida na kati ya hizo Tsh 89,196,000.00 ni fidia ya vyanzo vilivyofutwa.

Akiendelea kuwasilisha mapendekezo ya bajeti Ndg Kaijage ameelezea mikakati iliyowekwa ya  kuhakiksha mapato yanakusanywa katika mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kupitia upya mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa mapato kwa kuboresha maeneo ambayo yana mapungufu,kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kukusanya mapato,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini mianya inayovujisha mapato,kupitia upya sheria ndogo za mapato na kutumia mifumo ya ki-electronic katika vyanzo vyote vya mapato.

Akichangia hoja mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Ndg Ismail Ismail ameipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa soko la kisasa sambamba na ukarabati wa mto kikundi na kushauri eneo la kikundi palipouzwa viwanja kuna eneo lilibaki lijazwe kifusi na litumike kama stendi ya bajaji ili kusaidia usafiri kwa wafanyabiashara na wanunuzi watakaokuwa wanafika kupata bidhaa mbalimbali katika soko hilo.

Naye Ndg. Elizeus Rwegasira alitoa ushauri wa kupunguza bei pendekezwa ya vioski vya soko kuu ambapo vioski vya juu vimependekezwa kulipiwa Tsh 200,000.00 na vya chini Tsh 300,000.00 na kueleza endapo bei itakuwa kubwa wananchi watashindwa kupanga na vitabaki wazi na kuifanya Halmashauri kukosa mapato.

Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg Fikiri Juma ameshauri utengenezwe utaratibu wa  kuvua samaki katika bwawa la Mindu ili Halmashauri iweze kutoza wavuvi kwa utaratibu mzuri na kuepusha migogoro,na kushauri kijengwe kituo cha polisi katika kata ya Kihonda ambacho kitatoa huduma na hii ni kutokana na wingi wa wananchi wanaoishi katika kata hizo za pembezoni.

Mstahiki meya wa Manispaa amehahidi kuendelea kufuatilia urejeshwaji wa stendi ya Mabasi Msamvu ili Halmashauri iendelee kukusanya na hatimaye kuweza kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kwasasa kinachosubiriwa ni ushahidi wa picha za video zilizorekodiwa  wakati akitoa tamko hilo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa