• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

KATIBU MKUU KIJAZI ATETA NA VIONGOZI MOROGORO, ATOA MAAGIZO

Posted on: June 3rd, 2022

KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi Dk. Allan Kijazi ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Morogoro kufanya upya tathmini ya wadaiwa sugu wa mashamba makubwa Mkoani humo ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki kwa wamiliki wa mashamba hayo.

Dk. Kijazi ametoa agizo hilo Juni 3 Mwaka huu wakati wa ziara yake ya Kikazi ya siku moja ambayo pamoja na mambo mengine, ilikuwa na lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali za watumishi wa Idara ya Ardhi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo.

Katibu Mkuu katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, ameweka wazi kuwa kitendo cha baadhi ya wamiliki wa mashamba makubwa kutolipa madeni ya kodi ya pango la umiliki wa ardhi ni kuikosesha Serikali mapato halali na hivyo kuisababishia Serikeli hasara.

“Kwanza tupate takwimu kamili ya madai ya mashamba yote makubwa kwa Mkoa wa Morogoro, madeni tunayowadai ili tuweze kuchukua hatua mahususi kuhusu wamiliki wa mashamba haya” amesema Dk. Kijazi.

Sambamba na hayo Dk. Kijazi ameonya utaratibu wa wananchi kuvamia mashamba na maeneo yaliyo wazi au yasiyoendelezwa na baadae kuomba kupewa mashamba hayo ambapo baadhi ya wananchi huishia kuyauza maeneo hayo. Amesema, utaratibu huo hautakuwa na tija katika Taifa na hivyo Serikali inalazimika kukemea tabia hiyo na kuchukua hatua kali ili kulinda ardhi kwa manufaa mapana ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Anza-amen Ndossa amemuomba Katibu Mkuu huyo kusimamia kikamilifu matumizi ya ardhi ya Mkoa huo kwani Mkoa wa Morogoro kiuchumi na kimaendeleo unategemea ardhi kwa zaidi ya 90% kupitia kilimo na ufugaji hivyo kuendelea kuwa na migogoro ya ardhi Mkoani humo ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa Mkoa huo na taifa kwa jumla.

Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Mkoa wa Morogoro Frank Minzikuntwe amemuomba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kibali cha kutoa hati miliki za kimila kwa kutumia mfumo wa zamani ili kupunguza au kumaliza kabisa migogoro ya ardhi iliyopo baina ya mtu na mtu au jamii na jamii Mkoani humo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Ally Machela ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuikopesha fedha Halmashauri hiyo kwa ajili ya zoezi la kupima viwanja katika maeneo ya Kata ya Kihonda upande wa Kiegea STAR CITY ili kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi kwa haraka ambapo hadi sasa zaidi ya viwanja 3600 vimepimwa kupitia mkopo huo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa