• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

KATIBU MKUU TAMISEMI ATEMBELEA MABWENI YALIYOUNGUA NA MOTO SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA MOROGORO.

Posted on: July 11th, 2021

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe, amefanya ziara ya kutembelea katika Mabweni yaliyoungua na moto shule za Sekondari mbili ikiwemo shule ya Wasichana ya Kiislamu ya AT-TAAUN na Shule ya Sekondari Charlotte zilizopo Manispaa ya Morogoro.

Ziara hiyo imefanyika leo, Julai 11/ 2020 akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando, Kamati ya ulinzi na usalama , Kamanda wa Jeshi la ZimaMoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro , Goodluck Zelote, pamoja na Uongozi wa Manispaa ya Morogoro ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Pili Kitwana.

Katika ziara hiyo, Prof. Shemdoe, amesikitishwa na uharibifu wa moto ulioteketeza mali za wanafunzi huku akiwataka walimu, wanafunzi pamoja na Uongozi wa shule kuwa na subra katika kipindi hiki kifupi cha mpito.

Prof. Shemdoe, amewaomba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Morogoro washirikiane vyema katika kufanya kutathmini madhara yaliyojitokeza kutokana na moto huo ili Serikali iweze kuwa na taarifa kamili na kujua nini kinaweza kufanyika .

Mwisho, Prof. Shemdoe, amewataka wasimamizi wa Shule kuhakikisha wanafanya maboresho ya mifumo ya umeme mara kwa mara ili kuweza kuzuia majanga kama hayo kutokea.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Morogoro , amemshukuru Prof. Shemdoe kwa ziara yake na kuwatia moyo waalimu, wanafunzi pamoja na Uongozi wa Serikali.

DC Msando, amesema kuwa tayari wao kama Viongozi wa Serikali mara baada ya kupata taarifa ya kuungua kwa mabweni , wamechukua hatua ikiwemo ya kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafika eneo husika na kufanikisha kuuzima moto huo katika shule hizo mbili.

"Tumeona madhara yaliyotokea katika mabweni ya shule zetu, Jeshi la zimamoto limefanya kazi yake vizuri, nawapa pole sana, lakini kikubwa niwasisitize wasimamizi wa shule waendelee kuchukua tahadhari zote muhimu ili majanga kama haya yasijitokeze tena, naomba sana Uongozi wa Shule husika wawe na subra katika kipindi hiki cha uchunguzi naamini tukishajua chanzo ni nini , basi tutawapa taarifa sahihi juu ya nini kinapaswa kufanyika" Amesema DC Msando.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Charlotte , Sister Agness Wilson, amemshukuru Katibu wa TAMISEMI, Uongozi wa Mkoa , Wilaya na Manispaa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwa karibu sana na matatizo yaliyowakumba huku akisema ujio wa viongozi hao umewatia moyo wa kuendelea kufanya kazi .

" Tunawapongeza sana Viongozi wetu , ujio wao umetupa nguvu na matumaini, ukiangalia hapa madhara makubwa ni kuungua kwa vitu , moto huu ulitokea Julai 10, majira ya saa 3 asubuhi lakini tunamshukuru Mungu aliweza kutuepusha na janga hilo, hakuna aliyefariki wala kujeruhiwa, zaidi tu ni kuungua kwa bweni la kidato cha kwanza wasichana ambapo tukio hilo linatokea wao walikuwa madarasani, tukawahamisha wote ambao wamekutwa na majanga kuwaweka katika mabweni ya wanafunzi wa Pre- Form 1, lakini sasa tunaendelea vizuri  na wanafunzi wanasoma kama kawaida licha ya matatizo hayo" Amesema Sister Agness.

Shule ambazo mabweni yao yamepatwa kuunguliwa kwa moto ni pamoja na shule ya Kiislamu ya Wasichana ya AT-TAAUN iliyopo Kata ya Mji Mpya ambapo bweni la ghorofa ya juu yenye vyumba 6 vya madarasa vinavyobeba jumla ya wanafunzi 120, pamoja na Shule ya Sekondari Charlotte iliyopo Kata ya Tungi ambayo imeungua bweni moja la wanafunzi wa kidato cha kwanza upande wa wasichana.

Mpaka sasa jeshi la Polisi Wilaya ya Morogoro kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro wapo katika hatua za kufanya tathmini juu ya madhara yaliyosababishwa na janga hilo kisha baada ya kupata taarifa itawasilisha katika mamlaka ya juu ili kuona nini kinapaswa kufanyika.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa