WAKAZI wa Kata ya Mkundi, Lukobe pamoja na Tungi wapo katika hatua za mwisho wa kupatiwa majibu ya kilio chao cha maji kilichokuwa kikiwakabili kwa muda mrefu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Kituo cha kusukuma maji kilichopo Kata ya Kihonda eneo la Mizani ya zamani kinachosimamiwa na MORUWASA chini ya Mkandarasi Daino Tech Engineering Ltd Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara hiyo, RC Shigela, amesema Mkoa wa Morogoro licha ya kuwa na vyanzo vya maji lakini bbado wananchi uhaba wa maji ulikuwa ukitawala kwa kutegemea chanzo kimoja cha Bwawa la Mindu.
RC shigela,amesema ni wakati sasa wa Wakazi hao kuanza kufurahia matunda ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassani ya kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya Visima na vituo vya kusukuma maji vyenye thamani ya Zaidi ya Bilioni 1
“ Haya ni maeneo mapya hivyo tunatarajia mradi huu ukikamilika utaweza kuwahudumia wakazi wa Mkundi, Lukobe, na Tungi kwani ujenzi unaendelea kwa kasi na umefikia asilimia nzuri asilimia 40 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni 30/2022” Amesema RC Shigela.
Aidha, amesema mradi wa kisima cha tenki la maji umegahrimu Milioni 600, na kituo cha kusukuma maji umegharimu milioni 590 wenye pampu 2 na milioni 467 kwa ajili ya tenki lingine litakalo lisha wakazi wa Kilimanjaro na Tungi.
“ Rais wetu amedhamiria kumshusha mwanamke ndoo kichwani, Manispaa yetu ya Morogoro tumeokea kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 700 ambazo tayari zinaendelea kutumika, hata ule mradi Rais wetu aliosaini wa Tirioni 1 sisi Morogoro tupo na Mji wetu wa Ifakara wanaenda kunufaika nao, tunaamini mradi huu utakamilika mwezi Agosti na kilio cha maji katika maeneo niliyo yataja hapo juu tutakuwa hatuna tena changamoto hiyo ya maji” Ameongeza RC Shigela.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwakumbuka Manispaa ya Morogoro kwa kuwapatia fedha za mradi mkubwa wa maji ambao utaenda kuondoa kilio cha Wana Morogoro ikiwamo Tungi, Lukobe, Maeneo ya Kilimanjaro Kihonda pamoja na Tubuyu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa