• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA YAFANA MANISPAA YA MOROGORO.

Posted on: September 26th, 2024

MWENYEKITI wa Kamati ya Elimu, Afya na huduma za Uchumi Manispaa ya Morogoro , Mhe. Majuto Mbuguyu, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa kwa watoto waliopata ujauzito kupata elimu kama wanafunzi wengine lengo likiwa ni kuwasaidia watoto  wa kike kuendelea na masomo ili watimize ndoto zao.

Kauli hiyo ameitoa katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Septemba 25-2024 katika viwanja vya stendi ya zamani ya daladala Mjini kati akimwakilisha Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe.Pascal Kihanga.

"Nimpongeze Rais Dkt.Samia kwa kile alichokieleza kwamba watoto wa kike ambao wanakosa Elimu kwa kupata ujauzito wakishajifungua warudi darasani ili waendelee na utaratibu wa kupata Elimu kama wanafunzi wengine" Amesema Mhe Mbuguyu

katika maadhimsiho hayo,Mhe.Mbuguyu,amesema ipo haja sasa kila shule kuwepo na madarasa ya elimu ya watu wazima ili wale walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wapate fursa ya kusoma.

Kuhusu kuimarisha ustawi wa elimu ya watu wazima,Mhe. mbuguyu,amesisitiza kuendelea kuongeza majengo ya madarasa ya kimasomo ya ufundi stadi  ili kukabiliana na tatizo la ajira pamoja na  stadi za kujifunzia yaani kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK)  pamoja na kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendesha elimu ya watu wazima.

"Maafisa elimu wa Msingi na Sekondari tunawategemea kuanza kuchonoa mada za bajeti katika idara zenu,sisi baraza la madiwani kazi yetu ni kuidhinisha,kaeni pangeni leteni na hakika suala la kutenga bajeti likija kwetu sisi tutalipitisha ili tusiwavunje moyo hawa waalimu ambao wanafundisha watoto wetu" Ameongeza Mhe.Mbuguyu.

Nae Afisa Elimu watu wazima Sekondari Manispaa ya Morogoro, David Malimbwi,  amesema maadhimisho hayo yanalenga kutathmini shughuli za elimu ya watu wazima inavyoendeshwa katika Manispaa ya Morogoro kwa kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za  elimu ya watu wazima kwa kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanyika katika elimu hiyo.

Malimbwi,amesema kuwa serikali kupitia mpango wa elimu ya sekondari ulitoa fursa kwa wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwepo ujauzito na mazingira magumu waweza kujiunga na vituo vya elimu ya watu wazima. 

Pia amesisitiza kuwa wananchi wote ambao  walikosa kusoma  kwenye  mfumo rasmi wanatakiwa kujiunga katika vituo ambavyo vipo ndani ya Manispaa ya Morogoro ili waweze kupata uelewa wa kujua kusoma na Kuandika fursa ambayo italeta maendeleo kwa jamii na nchi nzima kwa ujumla.

Maadhimisho ya juma la Elimu ya watu wazima yamefanyika kwa mgeni rasmi kutembelea mabanda mbalimbali kutoka katika vyuo vya VETA, Vikundi mbalimbali na Banda la stadi za kujifunzia.

Maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 yamebeba kauli mbiu ya "Ujumuishi katika Elimu bila ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo” 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa