• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MAAFISA ELIMU KATA, WALIMU WAKUU WA SHULE TIMIZENI WAJIBU WENU-RC SANARE.

Posted on: July 3rd, 2020

Maafisa Elimu Kata na Walimu wakuu wa Shule za Msingi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa kusimamia kikamilifu ufundishaji ili kuinua kiwango cha ufulu wa Wanafunzi Shuleni.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, leo Julai 02,2020 wakati wa ziara ya kukagua shule pamoja na maandalizi yaliyofanywa baada ya kufunguliwa kwa shule hizo.

RC Sanare,  amesema ni jukumu la walimu Wakuu wa shule na Maafisa Elimu Kata kufanya ufuatiliaji wa karibu wa walimu ili kuhakikisha kuwa walimu hao wanatekeleza majukumu yao ya Ufundishaji vipindi mbalimbali Darasani kikamilifu.

Amesisitiza kuwa hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu Mwalimu mkuu,ama afisa Eimu Kata yoyote atakaethibitika kushindwa kutekeleza majukumu yake ya usimamizi na ufuatiliaji wa maendeleo ya Elimu katika eneo lake.

'"Nawaagiza Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule hakikisheni kuwa walimu wanafundisha kikamilifu na kumaliza mada mbalimbali zinazofundishwa mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi kujiandaa na mitihani kikamilifu, lakini kubwa zaidi hakikisheni kuwa mnadhibiti utoro mashuleni kwa kuhakikisha mnafuatilia kwa karibu Wanafunzi wanaoonekana kutofika shuleni pasipo kuwa na sababu za msingi""Amesema RC Sanare.

Katika hatua nyingine , RC Sanare, amewasisitiza Maafisa Elimu Kata na walimu wakuu wanadhibiti mimba za utotoni kwa kudumisha nidhamu kwa wanafunzi ili kuwanusuru watoto wa kike na athari za mimba za utotoni ambazo zimekuwa tishio kwa wanafunzi hao kutokana na kukatiza masomo.

Amesema ni jukumu la Maafisa Elimu Kata walimu wakuu wa shule na Wanajamii kwa ujumla kukemea tabia ya baadhi ya Wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi hao kukatiza masomo kwa kuishia kubeba uja uzito.

Amewataka Waalimu kutoa taarifa za Wanafunzi wajawazito kwenye mamlaka husika ili kusudi Serikali iweze kuchukua hatua dhidi ya wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu vya kuwakatiza wanafunzi wa kike masomo yao.

Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kuwachukulia hatua kali za kinidhamu baadhi ya Watendaji wanaonekana wanakwenda kinyume na utaratibu na sheria za kazi.

""Sisi tunafanya kazi kwa kuwahudumia wananchi, tunapokuja hapa sio kama hatuna kazi nyengine, lakini mbaya zaidi unafika eneo husika unaambiwa Mtendaji ana kazi nyengine, huu sio utaratibu ni nidhamu mbovu sana, wale ambao hawakufika katika mkutano wangu huu kesho mapema mjisalimishe kwa Mkurugenzi mkitoka na nipate taarifa jinsi walivyoshughulikiwa, hatuwezi kuleana kienyeji lazima tufuate sheria ili tunyooke na kuwatumikia wananchi wetu kwa kutoa huduma bora" Ameongeza RC Sanare.

Mbali na hapo, amekemea vikali kuwepo kwa zamu za kuingia madarasani kwa yale madarasa yenye mitihani huku akiwataka Waalimu wajipange vizuri kuhakikisha madarasa yote yenye mitihani ikiwamo darasa la Nne na la Saba wanaingia na kukaa madarasani kwa masaa yaliyoelekezwa na Wizara ya Elimu ya saa 11 jioni kama ilivyopangwa.

Katika kuhakikisha matokeo mazuri yanapatikana amehakikisha kwamba anaboresha madarasa ya TRC yaliyopo katika Manispaa ya Morogoro pamoja na kuwakabidhi Darasa la saba Shule ya Msingi Kikundi kiasi cha shilingi 300,000/= kwa ajili ya kununulia vifaa vya kufanyia mitihani.

Hata hivyo amewataka Waratibu elimu Kata , Waalimu kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya wataalmu wa afya katika shule zao wanazozisimamia katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

Mwisho amesisitizia wazazi kuchangia fedha kwa ajili ya watoto kuweza kupata chakula wanapokuwa shuleni ili waweze kusoma kwa bidii wakiwa wameshiba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bkari Msulwa, amewataka wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani yao.

“Mimi natamani sana matokeo yenu yakitoka nikiangalia Shule hizi ufaulu wa juu, , natamani sana na Mungu awabariki mpate matokeo mazuri huku mkimtanguliza Mwenyezi Mungu mbele,kikubwa zingatieni masomo na kuwaheshimu Walimu wenu” Amesema DC Msulwa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema katika kuhakikisha vituo vya mafunzo vya TRC vinaboreshwa ,atawasilisha taarifa CMT pamoja na kujadilina na idara ya elimu Msingi kuona jinsi watakavyoiweka katika Bajeti fedha za ukarabati wa vituo hivyo kwa ajili ya kunyanyua viwango vya ufaulu na taaluma kwa Shule za Manispaa ya Morogoro.

Miongoni mwa Shule alizotembelea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,Mhe. Loata Sanare ni pamoja na Shule ya Msingi Kikundi, Shule ya Msingi Kilakala na Shule ya Msingi Mwande .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa