• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA MANISPAA YA MOROGORO WAPATIWA MAFUNZO YA UBORESHAJI KAZI.

Posted on: September 19th, 2024

WATUMISHI wa Manispaa ya Morogoro kada ya watendaji wa Kata na Mitaa  wamepatiwa mafunzo elekezi  yatakayowasaidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi  ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu  katika maeneo yao ya utendaji kazi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali watu Manispaa ya Morogoro,,Pilly Kitwana, Septemba 19-2024 kwenye ukumbi wa Manispaa Ofisi Kuu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kitwana,amesema amewataka watendaji hao kuzingatia maelekezo yatakayotolewa ili wakayatumie katika kuboresha utendaji kazi wao kwa kuzingatia sheria kanuni na maadili ya kiutumushi.

“Jifunzeni vizuri ili mjue Sheria na Kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi wenu ili msiyumbishwe pale mnaposimamia utekelezaji wa kazi. Ikumbukwe watendaji ndio wasimamizi wa utekelezaji wa kazi na shughuli nyinginezo za maendeleo katika Kata na Mitaa yenu" Amesema Kitwana.

Akiwasilisha mada,Mhadhiri wa Chuo Cha Umma TPSC ,Gasper Kisinza, amefafanua kuwa, utumishi wa Umma unategemea nidhamu kubwa kwa watumishi ili kuepuka migogoro na muajiri itakayopelekea kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Gasper, amesema watumishi wanapaswa kufikia malengo ya kinidhamu ili kudumisha utumishi wenye weledi. Amesisitiza watumishi waepuke makosa makubwa na madogo ya kuitumishi ili kujiepusha na migogoro dhidi ya muajiri na jamii wanayoihudumia.

‘’Watumishi wa tuhakikishe tunazingatia kanuni za utendaji katika utumishi wa umma, ikiwemo kuzingatia masaa ya kazi, mahudhurio sahihi, kuzingatia kanuni na miongozo ya kazi katika jamii tunazoishi na mazingira tunayofanyia kazi. suala la upandishwaji vyeo, kuthibitishwa kazini pamoja na huduma nyingine za kiutumishi ni jukumu la muajiri kuendana na miongozo iliyowekwa” Amesema Kisinza.

Miongoni mwa mada zilizofundishwa ni dhana ya Utumishi wa Umma sheria,kanuni,miongozo na taratibu, Misingi ya maadiliya utendaji kazi katika utumishiwa Umma,majukumu na wajibu wa Maafisa Watendaji wa Kata,Usimamizi wa miradi ya Serikali, Ukusanyaji na utunzaji wa mapato ya Serikali, Misingi ya utoaji huduma bora kwa wananchi pamoja na mbinu za Kimenejimenti ya udhibiti na utatuzi wa migogoro katika ngazi ya Kata na Mitaa.

Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 1984, serikali iliporejesha mfumo wa serikali za mitaa, jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika katika kujenga mfumo imara wa kitaasisi ili kusimamia na kuratibu shughuli za utawala, utendaji na maendeleo katika ngazi ya mkoa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa