Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alidai uhuru wa Tanganyika ambapo mnamo usiku wa kuamkia tarehe 9 Desemba 1961 ,ilishushwa bendera ya Uingereza na kupanda Bendera ya Tanganyika na Mwalimu Nyerere akawa Waziri wa Kwanza.
Katika kupigania uhuru wa Tanganyika wapo waasisi ambao waliongozwa na Hayati Mwl. Nyerere lakini wengine washatangulia mbele za haki kwa hakika wangetamani sana kuiona siku hiyo na kuyashuhuda matunda ya jasho lao na kujitoa kwao wahanga kupigania uhuru ulipo leo hii, na kuona uhuru uliopiganiwa na kuweza kudumu kwa miaka 61 ya vizazi zaidi ya viwili. Siku ambayo ingewafanya kutazama nyuma na kufahamu hatua kubwa na kutokana na mafaniko yaliyopatikana na kutazama mbele kwa matumaini na ujasiri mkubwa kutokana na hatua zilizofikiwa leo hii.
Umuhimu wa siku hiyo ni wa kipekee kwani Jamhuri ya Muungano iliyopo sasa isingewezekana tarehe 26 Aprili 1964 kama pasingetanguliwa na uhuru wa Tanganyika na baadaye mapinduzi ya Zanzibar. Uhuru wa Tanganyika ulikuwa ni chachu na mchango muhimu sana katika kuwezesha mapinduzi matukufu ya Zanziba tarehe 12 Januari 1964.
Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeshuhudia mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu hususani barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, huduma za kiuchumi na kijamii, ujenzi wa madarasa, hospitali, zahanati na vituo vya afya, huduma za maji, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, pamoja na kuhamasisha uwekezaji na utalii.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imefanikisha kutekeleza ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni Soko Kuu la Kisasa lenye thamani ya Shilingi Bilioni 17.6, ujenzi wa mradi wa Stendi Mpya ya Daladala mafiga uliogharimu Shilingi Bilioni 5.2, Ukumbi wa DDC Mbaraka Mwinshehe wenye thamani ya Milioni 635, na Ujenzi wa Stendi ya Kaloleni uliogharimu Shilingi Milioni 644.
Manispaa imepanga kutumia jumla ya fedha kiasi cha Tshs. 14,894,034,000.00kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Kati ya fedha hizo kiasi cha Tshs. 5,778,989,000.00 ni fedha za mapato ya ndani, Tshs 5,014,326,000.00 ni fedha za serikali kuu na Tshs 4,100,719,000.00 ni fedha toka kwa wahisanina Jumla ya Tsh. 2,105,000,000.00 ni fedha zilizoletwa toka Serikali Kuu Nje ya Bajeti.
Hadi kufikia Septemba, 2022, fedha za miradi zilizopokelewa toka Serikali Kuu, Halmashauri na Wahisani ni Tshs.1,170,883,972.00 ambapo kati ya hizomchango wa Halmashauri ni Tshs. 670,883,972.00 ( Mapato ya ndani), Tshs.500,000,000.00 (S/ Kuu) ndani ya bajetina fedha toka Serikali kuu ni Tshs. 2,105,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo.
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA KIPINDI CHA JULAI-SEPTEMBA, 2022.
Katika kipindi cha Julai – Septemba, 2022 Halmashauri imefanikiwa kutekeleza bajeti ya miradi ya mwaka wa fedha2022/2023 kwa asilimia 36.2.
Kuhusu Miundombinu ya Halmamashauri, Manispaa imepanga kutumia shilingi Milioni 419,157,500.00 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.
Jumla ya Shilingi milioni 103,122,486.06 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha uwekaji wa Taa za barabarani na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.
Umaliziaji wa vyumba vya madarasa Shule za Sekondari, Halmashauri imeshatoa jumla ya Shilingi milioni 21 na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.
Katika kuona Manispaa inaongeza makusanyo yake, kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Halmashauri imepanga kutumia Milioni 150,000,000.00 na imeshatoa Shilingi Milioni 50,000,000.00 kwa ajili ya kununua Mashine 150 za kukusanyia mapato na karatasi zake (POS).
Katika suala la usafi wa Mji, Manispaa ya Morogoro, imepanga kutumia kiasi cha Shilingi Milioni 36 kwa ajili ya ununuzi wa mapipa 30 yenye ujazo wa kati kwa ajili ya kukusanyia taka.
Uboreshaji wa Masoko, Halmashauri, imepanga kutumia shilingi Milioni 200,000,000.00 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Masoko mawili ( Mawenzi na Mjimpya).
Katika kuwainua Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu, Manispaa ya Morogoro kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ,imetoa jumla ya Shilingi Milioni 964,831,500.00 kwa ajili ya Mikopo ya asilimi 10 ya mapato ya ndani.
Katika Sekta ya Elimu Sekondari, Manispaa imepokea fedha za mpango wamaendeleo ya UVIKO-19 jumla ya Tsh.1,720,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Sekondari pamoja na viti 4300 na meza 4300 kwa shule 21 za Serikali ikiwa 17 ni shule zilizokuwepo na 4 zimejengwa mpyaambayo kwa kiasi kikubwa madarasa hayo yameweza kupunguza Msongamano darasani katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona lakini kusaidia wanafunzi kujifunza vizuri darasani.
Lakini ujenzi wa madarasa haya ni wazi kuwa utulivu utapatikana kwa wanafunzi kwani zamani unakuta darasa moja ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 150, hali ambayo ilikuwa inapoteza utulivu kwa walimu.
Pongezi kubwa ziende kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza mpango wa ujenzi wa madarasa, Viongozi wa Chama na Serikali, pamoja na watumishi wote walioshiriki kwa namna moja ya kufanikisha mpango huo.
Manispaa kwa kuangalia mtawanyiko wa maeno yake ya kiutawala na kufaulu iliweza kuanzisha ujenzi wa shule mpya 4 za Mazimbu, Tungi, Mbuyuni na Mkundi pamoja na vyoo vya shule zote 4, ambapo hadi sasa shule hizo 4 mpya zimepata usajili na zimefunguliwa na kuanza kutumika na kufanya mradi huo
Kupitia fedha za mradi toka Serikali Kuu (SEQUIP) chini ya Uongozi wa awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Manispaa ilipokea kiasi cha shilingi Tsh. 940,000,000.00 kati ya 1,200,000,000.00 kwa jili ya ujenzi wa shule mpya nyengine 2 za Mindu na Lukobe kwa lengo la kuboresha miundombinu ya elimu Sekondari ndani ya Manispaa ambapo ujenzi wa madarasa 16 , maabara 6, maktaba 2, vyumba 2 vya TEHAMA, Majengo 2 ya Utawala na Vyoo matundu 40.
Katika mapato ya ndani , mwaka huu wa fedha 2022/2023 Manispaa imeweza kumalizia maboma 28 ya Sekondari ambayo yalikuwa yameanza kujengwa kwa nguvu za Wananchi mpaka sasa Manispaa ipo katika hatua za ukamilishaji wa ujenzi wa shule mpya ya Sayansi -Boma ya Ghorofa yenye madarasa 15 kupitia fedha za mapato ya ndani ambapo jumla ya shilingi Tsh. 684,025,350 zimetumika katika ujenzi huo.
Hivi karibuni Manispaa imeopkea tena kiasi cha Shilingi Bilioni Bilioni1.8 ya fedha za ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa madarasa fedha hizo zimetolewa kwa mwezi Septemba kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha kwanza watakaoingia mwakani 2023.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kwamba Tsh. Milioni 1,620,000,000.00 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza 2023, Tsh milioni 209,379,241.00 zitatumika kwa ajili ya elimu bila malipo kwa shule za Msingi na Sekondari na Tsh. Milioni 40,736,00.00 zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Hii ni mara ya pili kupokea fedha ,ikumbukwe Manispaa ilipatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Uviko 19.
Katika Idara ya Elimu Msingi,Manispaa ya Morogoro ilipokea jumla ya Tsh. 80,000,000.00 fedha za UVIKO-19 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa bweni 1 la Watoto 80 wenye mahitaji maalum, ujenzi upo hatua za umaliziaji na umefanyika katika Shule ya Msingi Norto iliyopo Kata ya Kihonda ambapo katika kipindi cha mwaka 1 ,Manispaa imejenga madarasa 2 kupitia mapato ya ndani.
Upande wa Sekta ya Biashara, ,Manispaa ya Morogoro imeanza kutekeleza mpango wa kuwatoa Machinga barabarani kwa kuwajenga vibanda vya biashara katika maeneo mbalimbali.
Jumla ya vibanda 880 vimejengwa katika eneo la Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro . Aidha, Manispaa imekamilisha ujenzi wa vibanda 546 katika maeneo ya faya , mtaa mfupi , masika na Stendi ya Mazimbu ambapo Manispaa imetumia Tsh. 235,000,000.00 fedha za mapato ya ndani kujenga miundombinu hiyo.
Hata hivyo, Manispaa imeishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia Tsh.490,000,000.00 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya biashara za Machinga.
Kupitia Sekta ya Afya , Manispaa ilipokea jumla ya Tsh. 500,000,000.00 kama fedha za awamu ya kwanza kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ,ambapo hadi sasa jumla ya majengo 2 ya OPD na Maabara pamoja na kichomea taka ambapo ujenzi wake umekamilika.
Katika Ujenzi wa Kituo cha afya Lukobe, Manispaa ilipokea jumla ya Tsh. 250,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo kwa sasa uujenzi wa Kituo hicho cha afya umekamilika ikisubiriwa vifaa tiba kwa ajili ya kuanza kazi.
Upande wa huduma za afya, Manispaa ya Morogoro imekamilisha ujenzi wa Zahanati 6 ambapo jumla ya Shilingi 475,432,391.50/= zimetumika ambapo Milioni 379,554,891.50 sawa na asilimia 75 ni mapato ya ndani na asilimia 21 kutoka Serikali kuu.
Manispaa imetenga kutumia shilingi Milioni 200,000,000.00 kwa ajili ya kumalizia miundombinu ya Zahanati 4 za Mji Mkuu, Kauzeni, Mafiga na Kihonda na kufanya kuwa na jumla ya Zahanati 10 zilizojengwa kupitia mapato yake ya ndani.
Sekta ya Mipango Miji, Ardhi na Maliasili, Manispaa ya Morogoro imepokea mkopo wa jumla ya Tsh. 1,000,000,000.00 kutoka Wizara ya ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupima Ekari 4500 baada ya Wataalamu kuandika andiko la mradi wa upimaji wa ardhi. Aidha Manispaa imeishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha kupata fedha hizo na Halamshauri ya Manispaa na sasa mpango wa upimaji umekamilika na zoezi linaloendelea ni la uuzwaji wa Viwanja vilivyopimwa katika mradi wa eneo la Kiegea A & B (star City).
Mbali na fedha ilizokopa ,Manispaa imechangia jumla ya Tsh. 127,600,000.00 kwa ajili ya shughuli ya upimaji kiasi ambacho ni sehemu ya mchango wa Manispaa kwenye mradi wa upimaji wa Viwanja.
Mwisho, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inamshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasssan kwa jitihada zake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi nzima hususani kwa upendo na uwajibikaji wake katika kuiletea maendeleo Manispaa yetu na kupunguza mrundikano wa wanafunzi uliokuwepo kabla ya yeye kuingia madarakani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa