• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA MOROGORO KUANZA UJENZI WA SOKO KUU LA KISASA WAKATI WOWOTE

Posted on: January 24th, 2018

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imeweka mpango wa kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko kuu jipya kwa kutumia fedha za Mfuko wa uboreshaji wa  halmashauri na Miji (ULGSP) kwa gharama ya Sh bilioni 9.5 katika mwaka huu wa fedha, 2018/2019 .

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa Morogoro, John Mgalula alisema hayo wakati wa kikao malaumu cha bajeti cha baraza la madiwani wa halmashauri  kilichokuwa kikiongozwa na Mstahiki  Meya , Pascal Kihanga.

Mgalula aliwahakikishia madiwani akiwemo Daud Salum ambaye yeye na wenzake walihoji kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa soko jipya la kisasa kwani walikuwa wanahitaji baadaye kuwafahamisha wananchi walivyotekeleza ilani ya uchanguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

“ Nawahakikishia waheshimiwa madiwani kuwa ujenzi wa soko kuu jipya la kisasa , mchakato wake umefikia hatua nzuri na mwaka huu wa fedha ujenzi utaanza kwa awamu ya kwanza kwa kutumia fedha za Mfuko wa ULGSP kinachofanyika kwasasa ni taratibu za kutangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi huu zinaendelea” alisema Mgalula.

Kwa upande wake , Meya wa Manispaa  alisema , halmashauri katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 mpango mkakati uliowekwa ni pamoja na kuboresha sekta ya afya kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Sina, na Misongeni .

Pia alitaja uendelezaji na kuanzisha ujenzi wa zahanati za Mbuyuni, Sultani Area, Kibwe, Konga, Tungi , Kauzeni na Kiwanja cha Ndege , kuendeleza ujenzi wa hospitali ya wilaya na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Mafiga lengo ni kusongeza huduma za afya karibu na jamii.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa