• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA

Posted on: June 16th, 2022

MANISPAA ya  Morogoro imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika inayoazimishwa Afrika nzima kila ifikapo tarehe 16 Juni lengo ikiwa ni kukumbuka mauaji ya watoto yaliyofanyika huko SOWETO Afrika ya kusini mwaka 1976. Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990.

Maadhmisho hayo yamefanyika Juni 16/2022 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwembesongo Kata ya Mji Mpya yakiambatana na maandamano.

Akizungumza katika madhimisho hayo, Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, amesema kuwa maadhimisho hayo ni kukumbuka wanafunzi zaidi ya 10,000 waliandamana kupinga elimu duni na ya kibaguzi ya wakoloni ambapo wanafunzi 176 waliuawa katika maandamano hayo na mauaji hayo yalileta majonzi makubwa katika bara la Afrika na kusababisha kuwepo kwa siku hii ili kupinga vikali ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanalindwa na kupatiwa haki stahiki.

Mhe. Kihanga, amesema kuwa siku ya mtoto wa Afrika inawakumbusha watoto hatua ya kijasiri waliyoichukua watoto wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda haki zao.

"Siku hii ni siku ambayo imetukumbusha ujasiri wa watoto wa Afrika kusini katika kulinda haki zao, hatua hiyo imeonesha kuwa watoto wanaweza kuleta mabadiliko hata wakiwa na umri mdogo,hivyo siku hii huadhimishwa kwa maslahi mapana na kuwakumbusha wazazi/wazazi,wadau na serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto ipasavyo" Amesema Kihanga.

Aidha, ameishukuru Manispaa ya Morogoro kwa kuwathamini sana watoto kwa kufanya jitihada katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na kutekelezwa katika ngazi zote hususani kwa kuchukua uamuzi wa  kuunda Mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya mtaa na kata.

Naye Mratibu wa Dawati la Watoto Manispaa ya Morogoro ambaye pia ndiye mratibu wa maadhimisho hayo, Joyce Mugambi,amesema kuwa Manispaa imeunda kamati za ulinzi na usalama za wanawake na watoto katika kata 29 na kamati hizi zimekuwa zikielimisha jamii juu ya haki za wanawake na watoto pamoja na kuzilinda.

Mugambi, amesema kuwa watoto wa Manispaa ya Morogoro bado wanapitia changamoto mbalimbali zikiwemo za vitendo vya ukatili wa kimwili,kihisia,kiuchumi na kingono katika mazingira wanayoishi hivyo ameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kukemea vitendo vya dhidi ya watoto na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Regina Mwamba, anayesoma Shule ya Msingi Mafisa A, ameishukuru Manispaa ya Morogoro kwa kuadhimisha maadhimisho hayo huku akiwaomba Viongozi kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na kupata mahitaji yao ikiwamo fursa ya kusikilizwa,haki ya kuendelezwa,haki ya kuishi,haki kwa watoto wa kike kupata nafasi ya kushiriki michezo kama ilivyo kwa watoto wakiume na haki ya kulindwa.

Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani mwaka huu 2020 ni "TUIMARISHE ULINZI WA MTOTO , TOKOMEZA UKATILI DHIDI YAKE, JIANDAE KUHESABIWA"

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa