• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA HUKU WADAU, JAMII NA WAZAZI WAKIASWA KULINDA MAADILI NA ULINZI WA MTOTO

Posted on: June 17th, 2024

KATIKA Kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka, Wazazi na jamii kwa ujumla wametakiwa kushirikiana katika ulinzi wa mtoto kwa kuhakikisha wanatenga muda wa kuzungumza na watoto na kufahamu changamoto wanazopitia ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili na kuwasaidia kufikia malengo yao kwa maendeleo ya baadaye.


Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga akiwa mgeni rasmi  katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika  Ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Morogoro Juni 16/2024.


Mhe. Kihanga, amewaomba wazazi na jamii kutenga muda wa kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili na hiyo ni pamoja wazazi kuepuka migogoro ya kifamilia ili kumlinda mtoto dhidi msongo wa mawazo inayotokana na migogoro anayoishuhudia ndani ya familia hali inayopelekea baadhi ya watoto kujidhuru au kubadilika kitabia.

 

“Manispaa imeandaa maadhimisho haya kwa kushirikiana na wadau  ikiwa ni sehemu ya njia ya kupaza sauti na kuonesha utetezi wetu kwa watoto, Tunafanya kazi na watoto wanaoishi kwenye mazingira ya umasikini uliokithiri na mwaka huu tumejikita katika elimu jumuishi kwa mtoto ambayo lazima izingatie maarifa, maadili na stadi za kazi na kwa upande wa wazazi na jamii wanatakiwa kushirikiana bega kwa bega na watoto kwa kuhakikisha mustakabali wao unakuwa mzuri.” Amesema Kihanga.


Mwisho, Kihanga,  ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kushirikiana na Asasi mbalimbali katika kuhakikisha mtoto wa Afrika anakombolewa katika utumwa wa kifikra na uchumi na nyanja mbalimbali ili kuweza kujenga jamii iliyo bora.


Akifafanua kauli mbiu ya mwaka huu ya ‘Elimu Jumuishi kwa Watoto Kuzingatie Ujuzi, Maadili na Stadi za Kazi ,Mhe. Kihanga  amewataka wazazi na  Jamii Katika Kumsaidia Mtoto katika Kufikia Malengo yake kwa Maendeleo ya Baadaye.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba, amesema, maadhimisho hayo yataangazia jukumu la wazazi na walezi pamoja na jamii kwa ujumla katika maendeleo ya mtoto kupitia elimu.

“ Majadiliano yataangazia masuala ya ujuzi, maadili pamoja na stadi za kazi na hii ni pamoja na kuhimiza jamii kuwaongoza watoto katika kutafikia mafanikio yao hapo baadaye.” Amesema Komba.

Komba, amewashukuru wadau wote , wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha wa kuhakikisha maadhimisho ya Mtoto wa Afrika Duniani yanafanyika kikamilifu.

Aidha amesema wanazingatia muongozo wa Taifa unatoa mweleko wa namna ya kuwafundisha watoto dhidi ya mmomonyoko wa maadili na kumfanya mtoto aweze kusimama katika haki zake.

Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa kitengo cha Maendeleo ya Jamii anayehusika na Dawati la mtoto  Manispaa ya Morogoro , Joyce Mugambi,  amesema, wamejikita katika nyenzo ya elimu kwa kuwa humpatia mtoto mwanga, ujuzi na maarifa ya kuweza kutambua alipo na namna ya kupambana dhidi ya hali iliyopo kwa ubora wa baadaye.

Mugambi amesema katika kumwendeleza mtoto dawati hilo humsaidia mtoto katika shughuli za shule na jamii kwa ustawi wao kwa kuhakikisha analindwa katika kufikia ndoto zao.

Aidha, Mugambi amesema, kupitia mabaraza ya watoto, majukwaa na klabu za watoto wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kuhusiana ma malezi, utu wema, uongozi na maadili ili kuwalinda dhidi ya mabadiliko ya teknolojia katika makuzi yao.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa