• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAANZA ZOEZI LA UUZAJI VIWANJA , RC MWASA AWAKALIA KOONI VISHOKA

Posted on: December 1st, 2022

WAKATI Manispaa ya Morogoro ikianza rasmi zoezi la uuzwaji wa Viwanja eneo la Kiegea A na B Star City mara baada ya kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa, amepiga marufuku madalali wa uuzwaji wa Viwanja (Vishoka) ambao wamekuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, ameitoa Novemba 30/2022 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mpango wa kutangaza na kukabidhi Viwanja vilivyopimwa na Manispaa ya Morogoro eneo la Star City Kiegea.

Akizungumza katika uzinduzi huo, RC Mwassa, amewataka wananchi watakaopewa fidia na wale watakaonunua Viwanja marufuku kuuza kiholela Viwanja hivyo kwani kufanya hivyo kunasababisha migogoro ya ardhi.

Aidha, RC Mwassa, amesema mwananchi yeyote atakayetaka kuuza Viwanja vyake lazima awasilishe maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ikiwa imeonyesha orodha ya Viwanja anavyokusudia kuviuza.

“Migogoro imeisha, wale mabingwa wa kuuza viwanja bila kufuata utarartibu iwe mwanzo na mwisho, vishoka nitakula nakula sahani moja,lazima madalali wa viwanja tuwaondoe, haiwezekani tumetumia nguvu kubwa ya kutatua mgogoro wao waanziishe upya hili sitalivumilia, niombe Manispaa hiki ni chanzo kipya cha mapato, hakikisheni fedha za wananchi ziingizwe moja kwa moja kwenye akaunti yake wakati wa mauzo ambayo ataiwasilisha Manispaa wakati wa uundaji mkataba” Amesema RC Mwassa.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Masando,amesema kwa sasa Mji unahitaji kupangwa hivyo wananchi lazima wasikilize maelekezo na maagizo ya Viongozi badala ya kukiuka maagizo hayo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela,amesema katika mchanganuo wa matumizi ya viwanja , viwanja 7946 vimerejeshwa kwa wananchi na ambapo katika viwanja 3965 vilivyobaki Manispaa ,mchanganuo wa matumizi yake ni eneo la makazi Viwanja 2,740, Makazi na Biashara 915, Huduma (Shule, Zahanati, Vituo vya afya n.k) 147, Biashara 36, Viwanda Vidogo 68 na Maeneo ya wazi (POS) na Viwanja vya Michezo 59, na hii ni baada ya mgawanyo wa makubaliano ya kugawana asilimia 55 kwa wananchi na Manispaa kupata asimia 45.

Zoezi la Ugawaji wa Fomu za mauzo ya Viwanja litaanza kufanyika Tarehe 5/12/2022 katika Ofisi za Ardhi zilizopo Stendi Mpya ya Daladala Mafiga ambapo kwa malipo ya ununuzi ya Viwanja yatafanyika kwa awamu moja ndani ya miezi 3 na bei ya fomu ni shilingi elfu 20.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa