• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAKABIDHI VIBAO 29 VYA UPIMAJI VIASHIRIA VYA LISHE KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 5

Posted on: May 31st, 2023

MANISPAA ya Morogoro imewakabidhi watoa huduma wa Kliniki ya afya ya uzazi,Baba, mama na Mtoto vibao 29 kwa ajili ya kupima viashiria vya lishe kwa Watoto chini ya miaka 5.

Vibao hivyo vimegaiwa Mei 30/2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Shabani Duru, katika ukumbi wa Soko Kuu la Chifu kingalu Morogoro.

Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo kwa watoa huduma hao, Duru, amesema ujio wa vibao hivyo utasaidia kwa kiasi kikubwa Kliniki kupima viashiria vya lishe kinachoainisha urefu/kimo na umri ( udumavu) kwa Watoto chini ya miaka 5.

Duru amesema, athari za udumavu ni nyingi ambazo hupelekea Watoto kuwa hatarini kupata magonjwa sugu Kama moyo, saratani na mengineyo.

" Udumavu unawapa mzigo mkubwa wakiwa wakubwa katika kufikiri, uwezo wa kuchambua mambo, kutafakari kwake na hata kuelewa kwake masomo darasani, Kuna wakati unaweza kumchapa na kumpa adhabu Kali Mtoto darasani ukadhani anafanya makusudi kutoelewa kile anachofundishwa , kumbe akili yake ilidumaa kwa kukosa lishe tangu utotoni" Amesema Duru.

Mwisho, amewataka watoa huduma wa afya kutoa huduma kwa weledi na kutunza vifaa vizuri ili kuendelea kuboresha afya, lishe na ustawi wa Wananchi wa Manispaa ya Morogoro.

Kwa upande wa Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Reinfrida Isack, akimwakilisha mganga mkuu Manispaa,amesema Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa sehemu zenye udumavu kwa asilimia 26.4 kufuatana na tafiti za lishe kwa TNNS, 2018.

" Upatikanaji wa vibao hivyo vitasaidia kujua Watoto wenye udumavu na kuweza Kuandaa afua sahihi katika kukabiliana na udumavu na kuweza kujipima wapi tunatoka na wapi tunakwenda" Amesema Rainfrida.

Naye Afisa lishe Manispaa ya Morogoro, Jackline Mashurano amesema Manispaa imekuwa na changamoto  katika mfumo wa afya wa taarifa ( DHIS2) juu ya taarifa ya uwiano wa urefu na umri chini ya miaka 5, hivyo vibao 29 vya kuanzia vitaongeza na kuboresha utoaji wa huduma na kurahisisha upatikanaji wa taarifa zitakazo anzia katika kitabu namba 7 Cha Watoto na baadae kuingizwa katika mfumo.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa