MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema katika kipindi cha mwezi mmoja Manispaa imeweza kutekeleza ujenzi wa madarasa 10 ya shule za Msingi kupitia mapato ya ndani.
Akizungumza juu ya ujenzi huo, Machela, amesema madarasa hayo hadi kukamilika kwake yametumia zaidi ya shilingi milioni 220 ambapo kwa sasa yameshaanza kutumika.
Machela, amesema ujenzi wa madarasa hayo ulianza Septemba 4 na kukamilika Septemba 30 /2022 , huku akisema Manispaa itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ukiachilia ujenzi wa madarasa.
" Tumekamilisha madarasa 10 ambayo kwa sasa yanatumika , fedha hizi ni mapato ya ndani ya bajeti yetu ya mwaka 2022-2023, nilishukuru Baraza la Madiwani kwa kusimamia vyema na kupitisha fedha hizi ili kuendelea kutoa huduma bora ya elimu, hatutaishia hapa tuna miradi mingine ambayo tunaendelea kutekeleza kupitia mapato yetu ya ndani ikiwamo miradi ya afya " Amesema Machela.
Hata hivyo, amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023, Manispaa imejipanga kujenga madarasa 50 ya Shule za Msingi kupitia fedha za mapato ya ndani ambapo hadi kufikia Julai 30/2023, itakuwa imekamilisha ujenzi wa vyumba vyote vya madarasa na miundombinu yote muhimu ya elimu na afya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa