KATIKA kuhakikisha inapunguza ama kumaliza kabisa kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika manispaa ya Morogoro , imeamua kununua "greda" kutokana na pesa za makusanyo ya ndani.
Mhe.Kihanga,akiwa mbele ya baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Manispaa na mwakilishi wa kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa mitambo hiyo ya MANTRAC TANZANIA LIMITED, Collin Anamiah , amesisitiza utunzaji wa mitambo hiyo ili kuendelea kuinufaisha Manispaa hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo, amewashukuru wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwa kulipa kodi zilizowezesha ununuzi wa greda hilo.
"Greda hili Mstahiki Meya ni lao,sasa, Manispaa ya Morogoro tutembee kifua mbele maana mambo mazuri yanakuja, nitumie tu nafasi hii tu kuwataka wananchi wenzangu wa Manispaa ya Morogoro kulipa kodi wasikwepe maana manufaa tunayaona".Amesema Mkongo.
Greda hilo linatarajiwa kuwasili manispaa ya Morogoro katikati ya mwezi Desemba 2024 , litakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa maeneo ambayo yana changamoto za miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo yenye jumla ya kata 29.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa