• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAZINDUA KAMPENI YA USAFI MAENEO YA SHULE NA MAKAZI YA WATU

Posted on: May 16th, 2020

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro, imezindua rasmi kampeni ya usafi na mazingira katika maeneo za shule pamoja na makazi ya watu.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo Mei 16,2020 na Afisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako kwenye Shule ya Msingi Mafisa ''A'' Kata ya Mwembesongo.


Akizungumza na Waandishi wa habari, Kipako, amesema Manispaa imeamua kujiwekea utaratibu wa kuanzisha Kampeni hii ya usafi ambayo itakwenda moja kwa moja ikiwa na malengo ya kumshirikisha kila Mwananchi anayeishi Manispaa ya Morogoro pamoja na Kata zote kuhakikisha anashiriki katika shughuli za usafi.


Amesema kuwa lengo la kuanza katika maeneo ya shule ni kutokana na shule kukosa wanafunzi kufuatia likizo ya Serikali baada ya kuingia kwa Janga la ugonjwa wa CORONA , hivyo maeneo mengi ya shule yamegeuka vichaka jambo ambalo ni hatarishi kufanya maeoeno hayo kuwa kificho cha wadudu wakali pamoja na kuweka mazalia ya mbu na kusababisha magonjwa kwa jamii kama vile Malaria.



Kipako , amesema kuwa Manispaa ya Morogoro kupitia Idara ya Mazingira itaunda kikosi kazi ambacho kitaongozwa na Afisa Mazingira wa Manispaa kwa ajili ya kuendesha kampeni ya usafi kwa kupitia Kata moja badala ya nyengine.


“ Nimshukuru sana Mkurugenzi wetu wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba kuja na wazo zuri sana pamoja na Afisa Mazingira wetu wa Manispaa kwa jitihada mbali mbali za kupambana na suala la usafi , baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wetu wa manispaa , tulikaa vikao tuka kubaliana na kushusha maelekezo kwa Watendaji wote wa Kata kwamba tunaanza Kampeni ya usafi , kubwa zaidi nimefurahishwa sana kuona kampeni hii wananchi wameipoke kwa bashasha sana , nawapongeza sana Watendaji wa kata , watendaji wa Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa hapa Mwembesongo kwa uhamasishaji wao ambapo tumeona wananchi, kamati za shule, walimu wa shule , wameitikia wito na kutuunga mkono, hatutaishia hapa leo tumezindua na tunatarajia kampeni hii kuwa ya kipekee kwani imezingatia maeneo yote yaliyopo ndani ya Manispaa tuendelee kushikamana kwa pamoja tutafanikiwa na Manispaa yetu itakuwa ya mfano kwa usafi ‘’ Amesema Kipako.

‘’Kampeni hii tutafika nyumba kwa nyumba, Mtaa kwa mtaa, Kata kwa Kata , na wale ambao watashindwa kuendana na kasi ya usafi wa Mazingira ndani ya Manispaa yetu iwe wananchi au watendaji watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kushindwa kufikia malengo, kikubwa wananchi wafanye usafi na waweke taka sehemu elekezi huku sisi kazi yetu ikiwa ni kupitia na kuzikusanya kuzipeleka dampo , tukishirikiana kwa pamoja changamoto ya usafi katika Manispaa yetu itabaki historia “” Ameongeza Kipako.

Hata hivyo, amewaagiza Watendaji wa Kata, Mitaa, Maafisa afya pamoja na wananchi waliopo ndani ya Manispaa waibebe kampeni hii na kuichukulia kwa uzio wa hali ya juu sana katika maeneo yao ili yale malengo tarajiwa yaweze kutimia.


Amesema matarajio yake ni kuona Kampeni hiyo inafanikiwa kwa asilimia 100 ili yaendane na malengo yaliyokusudiwa katika kupata matokeo chanya yatakayoifanya Manispaa kung’ara katika suala zima la usafi ambalo limeonekana kuwa changamoto.

Kwa upande wa Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro , Dauson Jeremia, amesema kampeni hiyo ya usafi italenga katika kusimamia mifereji yote inayozunguka biashara, soko, Viwanda, makazi ya watu, shule pamoja na ofisi ikiwemo ukaguzi wa nyasi ndefu katika maeneo hayo.


‘’Tumezindua rasmi kampeni yetu ya usafi tukianza na maeneo ya shule, lakini hatutaishia hapa pia tutakuwa na operesheni ya kuangalia wale watu ambao wanaotupa na kumwaga takataka katika mtaa, mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni au mahali popote hadharani au katika eneo lolote la wazi bila idhini ya Halmashauri na kuweza kuwachukulia hatua kali za kisheria “ Amesema Jeremia.

Amesema kampeni hiyo itakuwa na malengo ya kumshirikisha kila Mwananchi anayeishi Manispaa ya Morogoro pamoja na Kata zote kuhakikisha anashiriki katika shughuli za usafi.


Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mwembesongo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mipango miji Manispaa ya Morogoro, Mhe. Ally Kalungwana, ameipongeza Manispaa kwa kuja na wazo zuri ambalo linaweza kuwa suluhisho la changamoto ya usafi ndani ya Manispaa.

Amesema Kampeni hiyo wao wameipokea vizuri sana , na watahakikisha wanakuwa bega kwa bega ili kuona inafanikiwa na inazaa matunda.



Kalungwana , ametoa wito kwa Madiwani wa Manispaa ya Morogoro kuichukulia kampeni hiyo kama suluhisho la usafi ndani ya Manispaa na kuendelea kuhamasisha wananchi waweze kushiriki kikamilifu ili malengo yaliyotarajiwa yaweze kufikiwa.

“Tumeipokea vizuri sana kampeni hii, ni jambo zuri na la kiubunifu, nampongeza Mkurugenzi wetu anafanya kazi kubwa sana, idara ya mazingira na vikundi vya usafi, niwaombe wananchi wa Kata yangu tuipokee kwa uzito mkubwa na tushirikiane kikamilifu kwa ajili ya kuweka Kata yetu safi , nawapongeza sana wananchi walioitikia wito na kuja kutuunga mkono na tutashinda vita hii ya usafi na kuifanya Manispaa yetu isonge mbele” Amesema Mhe. Kalungwana.



Hata hivyo, amesema katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa ni vyema wananchi wakajitokeza kufanya usafi katika maeneo ya shule ili ziendelee kuwa na mazingira mazuri ili hata shule zikifunguliwa wanafunzi wasiingie katika adha kubwa ya kuminyana na mapori.

Naye mkazi wa Kata ya Mwembesongo, Bi. Sawita Haji Narani, amesema wao wameipokea kampeni hiyo kwa kishindo kikubwa sana na kuahidi ushirikiano mkubwa dhidi ya Serikali katika kusimamia usafi.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa