• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO ATAKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA LIENDESHWE KWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA TUME.

Posted on: January 27th, 2020

MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kuhakikisha wanaendesha zoezi hilo kwa mujibu wa Sheria , Kanuni pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ameyazungumza hayo, wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro leo Januari 27,2020.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amewapongeza washiriki wote walioteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi hilo muhimu la Uandikishaji wa Wapiga kura.

Amesema kuteuliwa kwao kumetokana na ujuzi, uwezo na uzoefu walionao katika kutekeleza majukumu ya Kitaifa likiwemo zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ambapo madhumuni ya mafunzo hayo ni juu  ya wajibu na taratibu za Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema kuwa mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa Uandikishaji yanalenga kuwawezesha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kupata uelewa wa jinsi ya kutumia kwa ufasaha BVR Kit kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura ili waweze kutoa mafunzo hayo kwa BVR Kit -Operators na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

"Matumani yangu baada ya mafunzo haya kila mmoja wenu atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kutekeleza wajibu na majukumu yake katika kufanikisha zoezi hili muhimu, pia nahakika baadhi yenu mlibahatika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kwa mara ya kwanza katika mfumo huu wa sasa wa Teknolojia ya BVR (Biometric Voters' Registration) mwaka 2015 hivyo mna uzoefu katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa zoezi hili" Amesema Sheilla.

Aidha, amewataka Maafisa hao kutumia uzoefu walionao kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa , kwa bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo na kuwafundisha wenzao ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi lililopita ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Pia amewaambia kwamba Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura na watazamaji wakati wa zoezi zima la uboreshaji ambao watapatiwa vibali maalum ambavyo vitawaruhusu kuingia katika vituo vya kuandikisha jambo ambalo ni muhimu na litasaidia kuleta uwazi katika zoezi hilo.

"Lazima mtambue kwamba , Mawakala wa Vyama Vya Siasa na Watazamaji hawatakiwi kuwaingilia watendaji mnapotekeleza wajibu wenu, hivyo maelekezo zaidi kuhusu suala hili yapo kwenye vitabu vya maelekezo mlivyopatiwa na ni muhimu kuyazingatia ili zoezi letu lifanyike kwa mujibu wa Sheria , kanuni na maelekezo" Ameongeza Sheilla.

Mbali na melekezo, amewaambia kuteuliwa kwao kumetokana na kuaminiwa hivyo wanauwezo wa kufanya kazi hiyo, kikubwa ni kujiamini na kujitambua na kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume ili waweze kufanya kazi wakati wa zoezi la Uandikishaji  pamoja na kufuata Sheria , kanuni, maelekezo na miongozo.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kuwataka watendaji kuhakikisha wanayajua na kuyatambua vyema maeneo watakayofanyia kazi ikiwemo miundombinu ya kufikia katika Kata na Vituo.

Hata hivyo, amesema katika kufanikisha zoezi hilo, kunahitajika ushirikianao mkubwa kati ya watendaji wote , Serikali , Vyama Vya Siasa na wadau wengine wote, pia waongeze ushirikiano mzuri wa karibu na Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro wakati wote watakapokuwa wanahitaji ufafanuzi au maelekezo katika kazi zao huku akiwatakia kazi njema katika mafunzo yao.

Kwa upande wa Kamishina wa Tume ya Uchaguzi, Marry Longway (Jaji Mstaafu) , amewataka Waandikishaji kuzingatia muda wakazi kabla ya saa  2:00 asubuhi wawe washafika katika vituo ili ifikapo saa 2:00 asubuhi kazi zianze kufanyika  ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea katika kazi nyengine za uzalishaji.

"Lazima ufike mapema, uangalie BVR Kit imefungwa, fomu zako zipo tayari , kalamu yako inaandika vizuri, sio inafika saa 2:00 asubuhi wewe ndio unafika unajisachi mfukoni peni haiandiki fomu hazionekani , BVR haijawashwa sio utaratibu lakini najua saa 12 jioni ndio muda wa kufunga kazi lakini lazima uangalie taarifa zako umezipangaje kwahiyo mkifuata hatua zote zoezi letu litakwenda vizuri bila matatizo na wananchi, mawakala wa Vyama Vya Siasa wala watazamaji" Amesema Longway.

Pia amewataka waandikishaji kuhakikisha wanawaandika majina na kuanza nao siku inayofuata kwa wale ambao muda wa kufunga kazi utawakauta wakiwa katika foleni ili kukwepa migongano na migogoro kwa wananchi.

Amesema vipaumbele vitolewa kwa Watu wazima, (Wazee), Watu wenye ulemavu, Wajawazito pamoja na wagonjwa hawaruhusiwi kukaa foleni.

Naye,  Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo, amewapongeza maafisa hao kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuifanya kazi kubwa ya kitaifa ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura.

Aidha amewataka maofisa hao kuwa wasikivu na kuzingatia mafunzo watakayopewa kuhusiana na uendeshaji wa zoezi hilo.

Hata hivyo Kombo  amesema hawatamvumilia mtu yoyote atakayekuwa mzembe wakati wa uboreshaji wa Daftari.

" Kama Manispaa yetu ya Morogoro tunataka tuwe watu wa kwanza kitaifa kuandikisha watu wengi zaidi na hii inawezekana tukiwa na weledi na tukizingatia mafunzo tutakayopewa" Amesema Kombo.

Zoezi la uboreshaji Daftari la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Morogoro linatarajiwa kuanza katika Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmshauri ya Mji wa Ifakara, Halmshauri za Wilaya ya Gairo, Kilombero, Kilosa, Morogoro na Mvomero kuanzia tarehe 03 hadi 09 Februari 2020.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa