SERIKALI ya mkoa wa Morogoro inatarajia kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali kubwa ya rufaa itakayokidhi utoaji wa huduma zote muhimu za wagonjwa baada ya kukabishiwa eneo la ekari 100 kutoka kwa wamiliki wa Dominion Plantation Ltd.
Wamiliki hao pia wametoa ekari nyingine 1,000 kwa ajili ya kujibu matatizo ya wananchi eneo la Tungi , Manispaa ya Morogoro ambao wamejenga makazi ya kudumu ndani ya shamba la mkonge linalomikikiwa kisheria ili waweze kupimiwa viwanja vya makazi .
Mshauri wa mradi wa Star City ,Dan Mrutu alisema hayo hivi wakati wa halfa ya makabidhiano ya ekari 100 zenye thamani ya dola milioni mbili kutoka kwa Dominioni Plantation kupitia Star City kwa Serikali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kujenga hospitali kubwa ya Rufaa ya mkoa.
Mrutu , alisema Dominioni Plantation inamiliki ekari 10,661 zilizokuwa zikilimwa zao mkonge ambapo kwa sasa imeanzishwa Kampuni ya Star Infrastucture Development (T), Ltd ambayo inasimamia masuala ya uwekezaji mkoani Morogoro, ( Special Economic Zone).
Alisema , chini ya mradi wa Star City ekari 1,100 zimetolewa kati ya hizo 100 kwa Serikali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kujenga hospitali kubwa ya Rufaa na nyingine 1,000 zimetolewa kujibu matatizo ya wananchi ambao wamejenga mkazi ya kudumu ndani ya shamba hilo linalimikikiwa kisheria.
Mshauri wa Mradi huyo alisema, baada ya kutolewa kwa ekari hizo , eneo la ekari 9,561zilizobaki litatumika katika shughuli za uwekezaji mkubwa wa viwanda, mahoteli , Vyuo vya Elimu na majengo ya kati ya kibiashara na ekari 500 kujengwa bandari kavu .
Akipokea ekari hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro , Dk Kebwe Stephen Kebwe , Katibu Tawala mkoa , Clifford Tandari aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa eneo hilo na kusema kuwa michoro ya hospitali hiyo ipo tayari.
Katibu Tawala wa mkoa huyo alisema , kujengwa kwa Hospitali ya Rufaa ya kisasa ya mkoa itaweza kupanua utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa haiwezi kutolewa .
Alisema ,miaka miwili iliyopita kulikuwepo na mwekezaji wa nje ambaye alihitaji kujenga Hospital ya kisasa ,lakini kutokana na ukosefu wa eneo alishindwa kufanya hivyo na kwa sasa milango ipo wazi kwa mwekezaji huo kuja kuwekeza .
Naye Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga licha ya kuwashukuru wamiliki wa Dominion , aliwataka kuharakisha kufanyika kwa marekebisho ya ramani ya kwa kuziondoa ekari 1,100 ili shughuli za upimaji viwanja na ujenzi wa miradi hiyo mikubwa iwenze kuanza mara moja.
“ Halmashauri haina kikwazo , tayari baraza la madiwani limepitia upimaji wa viwanja eneo hilo na kunachosibiriwa wezetu mrekebishe ramani yenu kwa kuziondoa hizi ekari kutoka ramani ya zamani” alisema Kihanga.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro , Dk Frank Jaccob alisema kutokana na ukubwa wa eneo hilo ,hospitali ya rufaa ya mkoa itakayojengwa inakidhi mahitaji yote muhimu katika utoaji huduma kwa wagongwa wa aina zote na eneo hilo pia litatumika kujenga vyuo vya utabibu , maabara na madaktari.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa mkoa , hospitali inayotumika sasa ya rufaa ni majengo yaliyokuwa ni makambi ya askari waliokuwa wamerejea nyumbani baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili mwaka 1945 na yamekuwa wakikarabatiwa mara kwa mara na kuongezwa kutokana na mahitaji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa