KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Abdalla Shaib Kaim amekagua na kuona, kuzindua pamoja na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo, yenye thamani ya shilingi 1,586,249,973.56, iliyotekelezwa na Halmasahauri ya Manispaa Morogoro
Ndugu Shaib amefanya hayo leo tarehe 13.05.2023 ambapo amezindua mradi mmoja wa maji safi na salama Kauzeni, kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ambayo ni kituo cha afya Tungi na jengo la utawala la shule ya sekondari Mkundi na kuona miradi minne ukiwemo mradi wa kutengeneza chaki wa OKOA Vijana Tungi, kitalu cha miche cha Madizini, kiwanda cha uchakataji wa taka ngumu za plastiki Msamvu na eneo la upandaji wa miti pembezoni mwa bwawa la Mindu.
Kando ya shughuli hizo, kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akiambatana na timu ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru pamoja na viongozi mbalimbali wameshirikiana na wananchi kufanya usafi katika soko la Mawenzi ikiwa ni kielelezo cha kuunga mkono Kauli Mbiu ya Mwenge huu wa Uhuru inayosisitiza utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa Morogoro umekimbizwa umbali wa kilomita 102.6 katika kata za Kauzeni, Boma, Tungi, Kihonda Maghorofani na Mkundi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa