• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

NAIBU MEYA MANISPAA YA MOROGORO AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA

Posted on: June 5th, 2021

Naibu meya  Manispaa ya Morogoro Mhe, Mohamedi Lukwele amewataka wananchi kuendelea kuhifadhi mazingira yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uharibifu wa mazingira na kuwataka  kupanda miti mingi hasa katika vyanzo vya maji.

Mhe. Lukwele ametoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya  mazingira Duniani yaliofanyika nje ya ukumbi wa DDC Manispaa ya Morogoro Juni 5, 2021 mara baada ya kufanya usafi na kupanda miti katika kingo za mto Morogoro.

Akizungumza na Wananchi ,Mhe Lukwele amewataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji na kuwasisitiza wakulima wa maeneo ya milimani kufuata sheria na taratibu wanazopewa na maafisa wa kilimo ilikufanya kilimo hicho kuwa na tija  bila kuharibu mazingira na kutokulima katika vyanzo vya maji.

Aidha,amewataka wananchi kuelimishana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mazingira na kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira na kutumia nishati mbadala ambayo haiaribu mazingira na kuathili viumbe hai.

‘’ Katika maadhimisho  ya mwaka huu 2021 kitaifa tunaongozwa na kauli mbiu inayosema "TUMIA NISHATI MBADALA ONGOA MIFUMO YA IKOLOJIA" maudhui ya ujumbe huu ni kuelimisha na kuhamasisha jamii kutumia  nishati mbadala ambayo ni  rafiki kwa mazingira yetu” Amesema Mhe, Mohamedi

Sambamba na maadhimisho hayo Mhe.Lukwele ametoa zawadi  ya fedha na vyeti kwa washindi wa usafi kwa Kata ambapo mshindi wa kwanza ni Kata ya Mafiga ambaye amepata shilingi Laki tano,kata ya Sabasaba wamepata shilingi Laki tatu, na Kata ya Mjimkuu wamepata shilingi laki mbili na kuwataka kutumia fedha kununulia vifaa vya usafi vitakavyotumika katika kata zao.

 Pia ametoa vyeti kwa Afisa Afya wa Kata ya Mafiga kwa usimamizi mzuri wa usafi,na kutoa cheti kwa kituo cha Afya Sabasaba,kikundi cha usafi Kajenjenjere na M2 smart,Cate Hotel,Benki ya NBC,shule ya sekondari Morogoro,shule ya sekondari Charlotte,Shule ya msingi Chief Albert na Carmel light.

Aidha kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro Ndg Jeremia Lubereje ambaye pia ni mchumi wa manispaa ya Morogoro ameendelea kusisitiza juu ya kushirikiana na Taasisi, wananchi wenye uelewa wa kuzifanya  taka kuwa mali hususani taka za plastiki na kutengeneza bidhaa yeyote yenye kuhifadhi mazingira.

"Kudhibiti utupaji holela wa taka ngumu na usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi,sisi kama Manispaa kupitia maafisa Afya waliopo katika Kata zote tumeendelea kuielimisha jamii kuacha kutupa taka hovyo, na  kupitia kampeni za usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tumekuwa tukipita kila kata kuhamasisha usafi wa mazingira"Amesema Lubeleje.

Hata hivyo , Afisa mazingira manispaa ya Morogoro Ndg. Dawson Jeremia amesema kuwa matumizi ya nishati isiyozingatia utunzi wa mazingira umesababisha kuwepo kwa changamoto nyingine ikiwemo upotevu wa viumbe hai, uharibifu wa ardhi, upotevu wa mimea asili na , upungufu wa upatikanaji wa maji na uzalishaji hafifu wa kilimo.

Aidha, amesema kuwa mpaka sasa Manispaa imeshirikiana na wadau wa mazingira wakiwemo RELEIGH, TFS, MORUWASA, BONDE kwa mwaka huu wa fedha2020/2021 kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali  ambapo jumla ya miti iliyopandwa ni 15,680, Katika maeneo ya taasisi za shule na vyanzo vya maji.

Maadhimisho haya yalianzishwa mwaka 1972 katika mji wa Stockholm Sweeden kwenye mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa kuhusu mazingira hivyo nchi mbalimbali zimekuwa zikiadhimisha siku ya Mazingira kwa ujumbe maaluu unaotolewa na umoja wa mataifa.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa