MASHINDANO ya UMISSETA Manispaa ya Morogoro yameanza rasmi katika viwanja vya shule za sekondari Morogoro.
Mashindano hayo yaliyo timua vumbi Mei 11/2023, yalishirikisha michezo kama vile soka, kikapu, mikono, riadha, wavu, table tenis kwa wavulana na wasichana, bao kwa wavulana na netiboli kwa wasichana.
Akifungua mashindano hayo ya UMISSETA, Mgeni Gerard, ambaye ndiye mgeni rasmi wa Mashindano hayo, amewaasa wanafunzi kutia nia na juhudi katika michezo hiyo kwani michezo ni afya na ajira kwani mashindano haya ni msingi wa vipaji vijavyo katika Taifa letu la Tanzania.
"Lengo la michezo hii ni kupata vijana wenye vipaji ambapo kama Taifa tunataka tuendeleze vipaji hivi na baadae tuwe na timu imara na kama ikiwezekana tushiriki katika mashindano mbalimbali ya AFCON na World Cup , hivyo amewaasa wanafunzi ambao wanashiriki mashindano hayo waongeze bidii na juhudi ili waweze kupata fursa ya ajira kwani hapo ndio sehemu nzuri ya kuonesha vipaji vyao" Amesema Mgeni.
Mgeni,amesema kuwa mashindano hayo yameshirikisha timu kutoka kanda 4 ambapo kanda hizo ni Bigwa Tungi, Kihonda, Mjini Kati pamoja na SUA.
Naye, Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro , Asteria Mwang'ombe, amesema lengo la mashindano hayo ni kuwandaa vyema wanafunzi na kupata vijana wenye vipaji ambao watashiriki ngazi ya Mkoa ili kuunda timu bora ya Mkoa wa Morogoro.
Sambamba na hayo, Mwang'ombe, amewataka wanafunzi hao wacheze kiufundi na kiustarabu ili wasije wakaumizana kwani baada ya michezo hii wanatakiwa kurudi shule na kuendelea na masomo.
"Lengo letu ni kuibua vipaji kwa vijana wetu hivyo nawaasa mkicheza mhakikishe mnacheza kiufundi na kiustarabu isije ikatokea kuumizana kwani baada ya mashindano haya mnatakiwa kuendelea na masomo kwani michezo ni mojawapo ya kuifanya akili yako kuwa imara kwahiyo baada ya hapa watakaochaguliwa inabidi mkaoneshe ujuzi wenu na wale ikatokea wamebaki wasikate tamaa warudi shule na wasome kwa bidii kwani michezo na elimu ni vitu vinavyoendana" Amesema Mwang'ombe.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa