Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amemuagiza Mkandarasi anayejenga mradi wa kituo cha mabasi madogo maarufu kama stendi ya daradara M/s NANDHRA ENGINEERING AND CONSTRUCTION COMPANY LTD kukamilisha kwa wakati ujenzi huo ili kuwaondolea kero wananchi na madereva wa mabasi hayo.
Mhandisi Kalobelo ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Morogoro na kueleza kuwa pamoja na kuridhika na Ujenzi wa Mradi wa Soko na kuhimiza ukamilishaji wa ujenzi wa soko hilo kwa wakati hali ilikuwa tofauti kwenye ujenzi wa kituo cha mabasi ambapo ilionekana kazi iliyofanyika kwa kipindi tangu mkandarasi alipoanza ujenzi kasi yake ni ndogo ukilinganisha na muda, hivyo akamtaka msimamizi wa Mkandarasi kuwepo eneo la mradi muda wote ili kuharakisha ujenzi huo.
“sasa la kwanza site manager wa Mkandarasi namtaka awepo hapa full time….Morogoro lazime tuwe na miradi ambayo tunaipanga iishe inaisha kwa wakati, na huu nataka uishe hata kabla ya muda mlioupanga” alisema Mhandisi Kalobero.
Pamoja na kumtaka Site Meneja kuwepo eneo la kazi muda wote, Mhandisi Kalobelo ameagiza wataalamu pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kukaa na Mkandarasi huyo ili kupunguza muda uliowekwa wa kukamilisha mradi huo kwa kuwa mda ni mrefu ukilinganisha na kazi iliyopo.
Halmashauri ya Manispaa iliamua kuibua mradi huo kutokana na hali halisi ya stendi iliyopo mjini kuzidiwa na wingi wa watu, magari na ukuaji wa Mji.
Mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi madogo ni mradi utakaochukua miezi 12 hadi kukamilika kwake ambapo na tayari umeanza kutekelezwa
Mradi huu unahusisha ujenzi wa jengo la Utawala, Vyoo, Maduka, soko dogo, migahawa, maegesho ya taxi, bajaji,pamoja na matanki ya maji na kufanya jumla ya gharama yote ya mradi kufikia zaidi ya Tsh. 5.2 Bil.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa