MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwasa, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Morogoro lengo ikiwa ni kuangalia namna miradi hiyo inatekelezwa huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Akiongea katika ziara hiyo RC Mwasa, ameipongeza Manispaa ya Morogoro, kwa utekelezaji wa miradi hiyo na kwa jinsi wanavyoshirikiana vyema baina ya viongozi wa Serikali na wa chama katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa ipaswavyo.
Aidha RC Mwasa, amesema ofisi yake itafanyia kazi maoni ya wananchi pamoja na viongozi ikiwa ni lengo la kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwa na maendeleo makubwa .
RC Mwasa, amesema amefurahishwa na ushirikiano alioupata wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo na amewataka watumishi wa Serikali na viongozi wote wa Manispaa kuendelea kushirikiana na kuwasisitiza kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato.
Pia RC Mwasa, amesisitiza viongozi wote wa Manispaa kufanya ufuatiliaji wa shughuli za miradi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kuendelea kusimamia usafi wa mazingira, kuendelea kuyalinda maeneo ambayo machinga wameondolewa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ziara yake na kuahidi kuwa maelekezo yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi na kutekelezwa ipaswavyo na kuhakikisha Wilaya ya Morogoro inaendelea kuwa ya mfano kwa nyanja zote.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Septemba 12/2022, RC Mwasa, ametembelea mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Ghorofa iliyopo Kata ya Boma, Ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Kata ya Tungi, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, mradi wa Pampu ya Maji Kihonda Mizani, Ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Lukobe, Shule mya ya Sekondari Lukobe pamoja na Shule mpya ya Sekondari ya Mindu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa