• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

TARURA MANISPAA MORO YAWATOA HOFU MADIWANI KUHUSU MATENGENEZO YA BARABARA

Posted on: October 31st, 2019

Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Manispaa ya Morogoro kwa mwaka wa fedha 2019/2020 umeidhinishiwa kiasi cha Sh bilioni 1.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi miwili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe.

Meneja wa TARURA, Manispaa ya Morogoro Mhandisi, Mnene James alisema hayo kwenye Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani la Manispaa  kilichofanyika Oktoba 31, 2019 kwenye ukumbi wa Manispaa.

Hata hivyo TARURA Manispaa ya Morogoro katika mwaka huu wa fedha iliwasilisha maombi ya miradi mitano iliyokuwa imeombea fedha kiasi cha Sh bilioni 1.9 .

Mhandisi James alisema hayo wakati wa kujibu swali la msingi la Diwani wa Kata ya Kihonda , Hamis Kilongo pamoja na hoja iliyotolewa na Diwani Zamoyoni Abdallah wa Kata Bigwa.

Madiwani hao kwa nyakati tofauti walimuuliza mstahiki Meya wa Manispaa , Pascal Kihanga kuhusiana na changamoto za ubovu wa barabara nyingi za Manispaa  licha ya uwepo wa TARURA .

Kwa mujibu wa Meneja wa TARURA Manispaa ya Morogoro kuwa , Manispaa ina jumla ya barabara zenye urefu wa zaidi ya kilometa 517 ambapo kwa nyakati hizi zipo kwenye hali mbaya.

Hata hivyo alisema , TARURA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha barabara hizo na kwa mwaka huu wa fedha ( 2019-2020) imeingia mikataba ya miradi miwili ya ujenzi wa barabara yenye kugharimu Sh bilioni 1.6.

Alisema , TARURA Manispaa ya Morogoro iliwasilisha miradi mitano na kuombea fedha kiasi cha Sh bilioni 1.9 , lakini ilipofika kipindi cha manunuzi yalitolewa maelekezo ya kupunguza asilimia 20 ya bajeti iliyoombwa ya miradi mitano na kubakiwa na miradi miwili yenye kugharimu Sh bilioni 1.6.

Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro alitaja baadhi ya barabara zilizopo katika mradi wa kwanza ni kata ya Boma , Mji Mkuu, Mbuyuni , Lugara – Lukobe , wakati mradi wa pili utahusisha kata ya Kihonda Magorofani, Kihonda- Mkundi, Mafisa na Mazimbu.

“ TARURA Manispaa ya Morogoro tayari imeziandikia kata husika barua ikizijulisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara wa kiwango cha changarawe “ alisema .

Pamoja na hayo alisema , TARURA itaendelea kutengeneza barabara za Manispaa  kila itapopata fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa barabara .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa