MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro Ally Machela amewataka wafanyabiashara kulipia Leseni za biashara, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kufungiwa biashara zao.
Ameyasema hayo Mei 23/2023 wakati akitoa maagizo kwa wataalam wa idara mbalimbalimbali kupita kwa kila mfanyabiashara ili kukagua iwapo mfanyabiashara husika anakibali kinachokubalika kisheria.
Aidha amesema iwapo itagundulika mfanyabiashara yeyote ambaye amekiuka agizo hilo basi hatua stahiki zitachukuliwa ambazo ni pamoja na kuamuru kufunga biashara kwa hiari yake au kufungiwa na wataalam kwa muda hadi pale atakapokidhi vigezo vya kuendele na biashara hiyo.
Kwa upande wa Afisa Mapato wa Manispaa Morogoro Fatma Lwebangira, amewataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa jopo hilo la wataalamu kwa kutoa maelezo sahihi juu ya uendeshaji wa biashara zao ili kurahisisha zoezi kutumia muda mfupi na kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Sanjari na kukagua vibali hivyo, jopo la wataalamu linaendelea kutoa elimu juu ya mfumo mpya wa tausi unaomsaida mfanyabiashara kusajili biashara yake kupitia mfumo huo ambao ni rahisi na wa muda mfupi ukilinganisha na utaratibu wa hapo awali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa