MKUU wa Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Dkt. Maneno Focus , amewataka waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi kuhakikisha wanawekeza katika mafunzo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kutoa huduma bora za afya kwa Wananchi.
Hayo amezungumza wakati wa kufungua Kikao kazi cha Maandalizi ya kuandaa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025-2026 katika ukumbi wa mikutao Msamvu Novemba 7-2024.
Dkt. Focus amesema waganga wafawidhi wanapaswa kuwekeza katika mafunzo kwa ajili ya maendeleo ya kitaalamu.
“Waganga wafawidhi wanapaswa kuwekeza katika mafunzo kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma ili kuhakikisha wanapata uelewa mpya na kuweza kwendana na mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya afya, mkifanya hivyo kutawawezesha wanaweza kutoa huduma bora na hasa za kisasa kwa jamii ya kitanzania katika maeneo yenu,”Amesema Dkt. Focus.
Aidha ametoa wito kwa waganga wafawidhi hao kila mmoja wao kujitoa kikamilifu katika kutekeleza majukumu na kuwa karibu na jamii wanayoihudumia.
Naye mdau wa masuala ya afya na Mratibu wa mradi wa TCI kutoka shirika la JHPIEGO Mkoa wa Morogoro, Tumaini Kiyola,amesema mradi wao umekuwa na mafanikio makuwa hususai kwenye afya ya uzazi wa mpango kabla ya mama kujifungua na baada ya kujifungua.
Maeneo yalitajwa kupewa vipaumele katika mpango wa bajeti katika vituo ni takwimu za wagonjwa kutoka DHIS 2,changamoto zinazotambuliwa na kamati za usimamizi wa vituo, hali ya utekelezaji wa maelekezo ya viogozi ngazi ya Manispaa ,Mkoa na Wizara ,vipaumele vya mpango wa kituo, hali ya upatikanaji wa rasilimali (watu,vifaa,vifaa tiba),mwenedo wa mapato a matumizi ya fedha za uchangiaji (user fee,ICHF,HIF) pamoja na kuwatambua wadau waliopo katika maeneo ya kituo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa