WASIMAMIZI wa Vituo vya kupigia kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27-2024 Manispaa ya Morogoro wamepatiwa mafunzo ili kuifanya kazi hiyo kwa uamakini na kufanya uchaguzi kuwa huru na haki.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Tanzanite Hall Novemba 22-2024 .
Aidha, wasimamizi hao wa vituo vya kupiga kura sambamba na mafunzo hayo waliyopatiwa pia wamekula viapo vya utii, uadilifu, uaminifu na kutunza siri wakati na baada ya zoezi hilo la uchaguzi.
Akizungumza na wasimamizi hao wa vituo vya kupiga kura,Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro ,Emmanuel Mkongo,amewataka wasimamizi wakawe makini hususani kwenye kujaza fomu za matokeo.
Mkongo,pia amewataka wasimamizi hao kuzingatia kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuufanya uchaguzi uende vizuri.
Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa linatarajiwa kufanyika tarehe 27-2024
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa