• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

WAZIRI JAFFO AWAAGIZA MAMENEJA WA TRA KUTOTOZA KODI MIRADI YA SERIKALI

Posted on: October 12th, 2017

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jaffo amewataka mameneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mikoani kuacha tabia za urasimu katika utoaji wa vyeti kwa wakandarasi wa barabara za halmashauri zinazojengwa kwa sasa.

Waziri Jaffo alitoa agizo hilo Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi ya barabara na shule za sekondari za Kilakala na Mzumbe ya wilayani Mvomero.

Jaffo alilazimika kutoa agizo hilo mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa meneja wa huduma za barabara mijini (TARURA) Bw Godwin Mpinzile aliyemlaumu meneja  wa TRA mkoa wa Morogoro Bi Kabuka Mwemezi kuwa amekuwa akichelewesha kuwapatia cheti cha ujenzi wa barabara kwa kumtaka kulipa kodi.

Baada ya malalamiko hayo Waziri Jaffo alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bw John Mgalula kumfuata meneja huyo na endapo ataendelea na msimamo wake atoe taarifa kwake ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Alisema baada ya Bunge kuondoa ongezeko la thamani VAT kwa baadhi ya vipengele bado kumekuwa na urasimu kwa baadhi ya mameneja wa TRA wa mikoa kwa kung'ang'ania na kuendelea kudai kulipwa kodi wakati ilishaondolewa.

Pia Waziri huyo aliwataka kandarasi wanaoendelea na ujenzi wa barabara za ndani za Halmashauri kuhakikisha zinakuwa kwenye kiwango chenye ubora kwani zimekuwa zikitumia fedha nyingi.

"Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara zilizoko ndani ya Halmashauri  ,sitaki kuskia ndani ya mwaka mmoja barabara imeharibika ,mkandarasi  atakaye haribu kazi ajue Serikali hii si ya kuchezea atachukuliwa hatua"alisema Jaffo.

Meneja wa TARURA Godwin Mpinzile alimhakikishia Waziri Jaffo kusimamia kikamilifu ujenzi wa barabara tatu za Nanenane ,Tubuyu zenye kilomita 2.4 na Maelewano yenye urefu wa mita 600 za Manispaa ya Morogoro na ujenzi huo unaghalimu kiasi cha shilingi 12.8 bilioni.

Ujenzi wa barabara hizo unafanywa kwa ushirikiano baina ya kampuni  mbili ya Group Six International na kampuni ya Lukolo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa