WENYEVITI wa mitaa wateule na wajumbe kutoka katika kata 29 za Manispaa ya Morogoro wameapishwa leo Novemba 28, 2024 katika Ukumbi wa Tanzanite Hall.
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi hao, Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Emmanuel Mkongo, amewatakia heri viongozi hao katika kazi zao na pia kawataka wakatimize kazi zao kwa uadilifu na kwa uaminifu mkubwa.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, amewataka Viongozi hao kuzingatia sheria taratibu na kanuni za nchi bila kukiuka maadili ya uongozi katika jamii na wametakiwa viongozi hao kuwa chachu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Sagara,amewataka viongozi hao kuwa walinzi wa amani na kuhakikisha wanazingatia viapo vyao kwa kuzisimamia sheria za nchi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zaidi kutenda haki kwa wanaowaongoza katika maeneo yao ya utawala.
Hakimu Mfawidhi ,Yonas John, amewapa nasaha viongozi hao kabla ya kiapo na kuwataka waheshimu na kuzingatia maudhui ya kiapo na kufanya kazi ya kuhudumia wananchi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za nchi.
”Kiapo hiki ni kwa mujibu wa sheria hivyo mnatakiwa kuheshimu kiapo hiki muda wote wa uongozi wenu.”Amesema Yonas
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa