MAJUKUMU YA IDARA.
1.Kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kanuni bora za kilimo chenye tija.
2.Kupanga na kusimamia utekelezaji wa malengo ya Kilimo kila mwaka.
3. Kusimamia upatikanaji wa pembejeo na zana bora za kilimo.
4 .Kuhamasisha uanzishwaji,usajili na kutoa mafunzo kwa vikundi vya wakulima kupitia mashamba darasa.
5. Kusimamia udhibiti wa visumbufu na magonjwa ya mimea.
6. Kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo ya kilimo chini ya idara.
7. Kuhamisha na kusimamia kilimo cha umwagiliaji wa asili na ulioboreshwa.
8. Kusimamia mpango wa matumizi bora ya ardhi.
9. Kusimamia vyama vya ushirika vilivyosajiliwa kuhusu shughuli zao na uendeshaji kwa mujibu wa sheria na kanuni za ushirika.
10. Kufanya ukaguzi wa shughuli za uendeshaji wa vyama vya ushirika.
11 .Kutatua migogoro kati ya wanachama na vyama vya ushirika inapojitokeza.
12. Kusimamia chaguzi za viongozi wa vyama vya ushirika.
13. Kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika.
14. Kukusanya na kutunza takwimu sahihi za vyama vya ushirika.
15. Kutoa elimu kwa wanachama wa vyama vya ushirika.
16. Kufufua vyama vya ushirika.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa