Ukaguzi wa Ndani
Utangulizi
Ukaguzi wa ndani ni kitengo huru, kinachofanya kazi za kushauri, kupendekeza, kuelekeza, kutadharisha, kuainisha viashilia hatarishi, kusaidia kuongeza thamani na kuboresha uendeshaji ili taasisi itimize malengo yake. Kitengo kinatoa taarifa za ukaguzi kwa mkurugenzi kila robo ya mwaka (Quarterly audit report)
Malengo/ Madhumuni
Kipengele Na. 28 cha Kanuni za Fedha za Umma (2004) na Mwongozo wa Ukaguzi wa Ndani kipengele cha 2.3 wa Mwaka 2013 inamtaka Afisa Masuuli kuanzisha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani. Madhumuni ya kitengo hiki ni kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya utumiaji mzuri wa rasilimali. Watu, fedha na mali. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:-
Mamlaka ya ukaguzi.
Ukaguzi wa ndani unafanyika kwa mamlaka aliyopewa Mkaguzi wa Ndani na Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Na. 9 ya mwaka 1982 Sehemu ya 45 (1) (iliyorekebishwa mwaka 2000), Memoranda ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2009 Agizo Namba 13(1)& 14(10), Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2001, Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 ya mwaka 2011 “International Professional Practice Framework” (IPPF) na Sheria ya Fedha za Umma Namba 6 ya mwaka 2001 (iliyorekebishwa mwaka 2010).
Huduma za ukaguzi zitolewazo na kitengo cha ukaguzi wandani.
Majukumu ya kitengo cha ukaguzi wa ndani ni:
1. Kukagua, kuthibiti na kutoa taarifa kama kuna udhibiti wa kutosha kwenye makusanyo, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za ofisi.
2. Kukagua na kutoa taarifa kama mifumo ya utendaji iliyoainishwa kwenye sheria , kanuni na maelekezo mbalimbali kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali yanafuatwa ili kuhakikisha kuwa kuna udhibiti wa kutosha kwenye matumizi fedha katika ofisi.
3. Kukagua na kutoa taarifa ya mipangilio na mgawanyo katika akaunti za mapato (revenue) na matumizi ni sahihi.
4. Kukagua na kutoa taarifa juu ya usahihi wa hesabu na taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na ofisi.
5. Kukagua na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo na inayotumika kutunza mali za serikali, pamoja na kufanya uhakiki wa mali hizo.
6. Kupitia na kutoa taarifa juu ya shughuli au mipango ya ofisi ili kuona kama inaendana na malengo na madhumuni ya uanzishwaji wa ofisi.
7. Kupitia na kutoa taarifa juu ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Menejimenti katika kujibu hoja za Mkaguzi wa Ndani; na kusaidia Menejimenti juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya hoja hizo; na pale inapofaa kusaidia namna ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
8. Kukagua mifumo ya TEKAMA iliyopo katika ofisi na kutoa taarifa kama kuna umadhubuti wa udhibiti uliopo.
9. Kuandaa Mpango kazi na Mpango mkakati wa ukaguzi.
10. Kuandaa na kusimamia mipango ya ukaguzi.
11. Kufanya ukaguzi wa thamani kwenye Miradi ya kimaendeleo na ukaguzi wa thamani mbalimbali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa