Manispaa ya Morogoro ni moja kati ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Morogoro. Ina Tarafa 1, kata 29 na mitaa 294. Halmashauri hii ina wakazi wapatao 471,409 ambapo wanaume ni 226,817 na 244,592 ni wanawake kwa mujibu wa maoteo yanayotokana na sensa ya mwaka 2022.
IDADI YA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA
Halmashauri ina jumla ya Vituo 92 vya kutolea huduma katika mgawanyo ufuatao:- Hospitali 5 (2- Serikali, 2- Taasisi za uma 1, binafsi ), Vituo vya Afya 15 (7 vya serikali,3 vya mashirika ya Dini (FBO) na 5 vya wau binafsi) kliniki 14, Zahanati 57 ( 25 Serikali,mashirika ya dini - 5, Binafsi 27 na Martenity home 1.
UTAWALA NA UONGOZI
Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe ina vitengo vitatu ikiwemo Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji wa huduma za Afya (CHMT’S). katika kuendesha shughuli zake.
Halmashauri ya Manispaa inayo Bodi ya Afya Pamoja na kamati za vituo zilizo hai katika kila kituo cha kutolea huduma za Afya ambazo zinafanya kazi kwa mujibu wa mwongozo. Kamati hizi zinasaidia kutatua changamoto nyingi toka kwenye jamii hali iliyopelekea kupunguza malalamiko ya wateja na kuimarika kwa utoaji wa huduma kwa ujumla.
Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe inafanya usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma ambapo jumla ya vituo 56 kati ya 92 vilitembelewa sawa na 61% kwa mwaka.
MFUMO WA GOTHOMIS
Ili kudhibiti upotevu wa mapato katika vituo Halmashauri inaendelea na ufungaji wa mfumo wa GOTHOMIS katika vituo vya kutolea huduma ya afya ambapo hadi sasa vituo vyenye mfumo huo ni 11 kati ya vituo 30 vinavyomilikiwa na serikali hii ni sawa na aslilima 34.5 Aidha Vituo 5 viko katika Hatua ya kufunga mfumo wa Got Homis ifikapo Juni 30, 2024 na Halmashauri imetenga kiasi cha Tsh milioni 37,800,000 katika mwaka wa fedha 2024/25 kukamilisha vituo vilivyobakia .
WATUMISHI
Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe ina Jumla ya watumishi 659 ambapo watumishi 3 wako kitengo cha Lishe, 19 ni Kitengo cha Ustawi wa Jamii na 628 wapo kitengo cha Huduma za Afya (Tiba na Kinga)
Aidha kuna upungufu wa kada mahsusi kama wataalamu wa dawa za usingizi (3), wataalamu wa kutengeneza meno bandia (8), wataalamu wa mionzi (8), data clerk (38), wataalamu wa macho.
Kwa mwaka 2022/2023 na 2023/2024 Halmashauri imepokea jumla watumishi wapya 55 ambao wamepangwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma.
FEDHA ZA MFUKO WA PAMOJA (BASKET FUND ZILIZOPOKELEWA KWA MWAKA 2023/2024.
NGAZI (COST CENTRE)
|
BAKAA 2022/2023
|
FEDHA ZILIZOPOKELEWA
|
FEDHA ZILIZOTUMIKA
|
FEDHA ZINAZOENDELEA NA MATUMIZI
|
CHMT
|
0
|
71,407,425.00 |
38,980,000.76 |
32,427,424.24 |
HOSPITALI
|
59,818,000. 75
|
119,022,375 |
122,819,576.82 |
56,020,798.18 |
VITUO VYA AFYA
|
27,392,829.88
|
156,626,346 |
133,032,179.20 |
50,986,996.68 |
ZAHANATI
|
53,650,378.31
|
135,460,682 |
127,449,884.75 |
61,661,175.56 |
TOTAL
|
140,861,207.00
|
482,516,828 |
422,281,641.53
|
201,096,394.66
|
MIRADI YA MAENDELEO
Halmashauri inaendeleza ujenzi wa miradi mbalimbali kama inavyoonesha kwenye Majedwali 2A na 2B hapo chini.
Jedwali Na. 2A: Mchango wa mapato ya ndani katika uendelezaji wa miundombinu ya Sekta ya Afya 2022 - 2024 yenye thamani ya Tsh.1,395,000,000.00
Na
|
JINA LA MRADI
|
ENEO ULIOPO (KATA)
|
FEDHA ZILIZO
POKELEWA |
HATUA ILIOFIKIWA
|
1.
|
KITUO CHA AFYA TUNGI
|
TUNGI
|
770,000,000
|
Hatua ya umaliziaji, OPD,RCH na walkway vimekamilika
|
2.
|
ZAHANATI YA KAUZENI
|
KAUZENI
|
140,000,000.00
|
Jengo la OPD Limekamilika na kuanza kutumika.
|
3.
|
ZAHANATI UWANJA WA TAIFA
|
UWANJA WA TAIFA
|
70,000,000.00
|
Jengo limekamilika na huduma za OPD zimeanza kutolewa
|
4.
|
ZAHANATI YA MLAPAKOLO (OPD NA MAABARA)
|
MJI MKUU
|
140,000,000.00
|
OPD na Maabara imekamilika na huduma zimeanza kutolewa.
|
5
|
ZAHANATI YA MAZIMBU
|
MAZIMBU
|
135,000,000.00
|
Jengo limekamilika huduma za awali zimeanza kutolewa.
|
6.
|
KIEGEA “B” (Ujenzi wa nyumba Mtumishi.
|
KIEGEA
|
100,000,000.00
|
Ujenzi hatua ya ukamilishaji nyumba ya mtumishi
|
7.
|
Ujenzi wa Maabara zahanati ya Kilakala
|
KILAKALA
|
40,000,000.00
|
Ujenzi iumekamilika
|
Jedwali Na. 2B. Fedha kutoka Serikali kuu yenye thamani ya Tsh 2,600,000,000/=
Na
|
JINA LA MRADI
|
KATA
|
FEDHA PO
KELEWA |
HATUA ILIOFIKIWA
|
3
|
HOSPITALI YA WILAYA(OPD,MAABARA WODI YA WAZAZI,MIONZI,DAWA,JENGO LA KUFULIA,WODI YA WANAUME,WODI YA WANAWAKE NA WODI YA WATOTO)
|
KIHONDA
|
2,000,000,000.00 |
OPD(100%) maternity,theatre(100%) na maabara(100%), bohari ya dawa(100%), mionzi(100%) na jengo la kufulia(100%).,Ujenzi wa wodi ya watoto,wanaume na wanawake ipo katika katika hatua za upauaji Hata Hivyohuduma kwa baadhi ya majengo zimeanza kutolewa.
|
4
|
KITUO CHA AFYA LUKOBE
|
LUKOBE
|
500,000,000.00 |
OPD, Maabara kichomea taka kimekamika 100%
Jengo la wazazi asilimia 84% laundry 99%.huduma za OPD zimeanza kutolewa. |
5
|
JENGO LA WAZAZI ZAHANATI YA KONGA
|
MZINGA
|
100,000,000.00 |
Hatua ya upakaji rangi
|
UTAYARI WA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika, unaosababisha mwili kupoteza maji mengi na kuishiwa nguvu hivyo unaweza kupelekea kifo. Ugonjwa huu unasababishwa na bakteria aina ya Vibrio.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ilianza kufanya maadalizi ya milipuko ya magonjwa (Emergency Preparedness plan), hii ilikuja baada ya mvua nyingi namilipuko ya kipindupindu kutoka maeneo menggi ya nchi.
HALI YA MLIPUKO
Tarehe 29.01.2024 halmashauri ya Manispaa Ya Morogoro iliripoti mgonjwa wa ugonjwa wa kipindupindu kutoka kata ya boma mtaa wa OLD DSM ROAD. aMpaka sasa tuna jumla ya wagonjwa/wahisiwa 57 na kifo kimoja vilivyothibitishwa.Aidha ufuatiliaji wa wahisiwa na waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa.
KAZI ZINAZOFANYIKA KUKABILIANA NA KIPINDUPINDU.
Kutoa elimu kwa jamii kupitia maafisa afya, watendaji na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kufanya Vikao vya kuimarisha timu za maafisa afya kutoa elimu ya afya na usimamizi wa usafi wa mazingira.
Kufanya ukaguzi wa afya na mazingira katika kata zenye maeneo Hatarishi zikiwemo Mafisa, Tungi, Mwembesongo Na Chamwino maeneo hatarishi ikiwemo stendi ya mafiga,soko la mawenzi.
Kutembelea, kukagua na kutoa elimu kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo shule, makanisa/misikiti.
Ukaguzi wa maeneo yote ya huduma ya chakula (migahawa,mama/baba lishe,hotel).
Kuzuia uuzaji holela wa vyakula,matunda ya kumenya, uuzaji wa ice cream, maji ya kandoro, mahindi ya kuchoma, na kupikwa, juisi ya matunda ya miwa na matunda bila utaratibu maalumu
kutoa elimu kinga na udhibiti kupitia gari la matangazo na radio.
Kugawa vidonge vya chlorine kwa wakazi wa mwembesongo,mafisa na kichangani pamoja na kata hatarishi.
MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KITENGO CHA WAGONJWA WA NJE (OPD) KWA KIPINDI CHA JANUARI 2023 HADI FEBRUARI 2024
Watoto chini ya miaka
|
Na
|
Watu wazima
|
|||||
Na
|
OPD Diagnoses
|
Number of Diagnoses
|
%
|
|
OPD Diagnoses
|
Number of Diagnoses
|
%
|
1.
|
Upper Respiratory Infections
|
26,463
|
36.13
|
1.
|
Upper Respiratory Infections
|
34,631
|
14.17
|
2.
|
Urinary Tract Infections
|
8,535
|
10.55
|
2.
|
Urinary Tract Infection
|
32,341
|
13.23
|
3.
|
Diarrhea with no Dehydration
|
7,120
|
8.80
|
3.
|
Ill Defined Symptoms (No Diagnosis)
|
19,599
|
8.02
|
4.
|
Pneumonia-Severe & Non-severe
|
5,198
|
6.42
|
4.
|
Hypertension
|
19,378
|
7.93
|
5.
|
Skin Infection, Non-Funga
|
4,601
|
5.69
|
5.
|
Peptic Ulcers
|
11,431
|
4.68
|
6.
|
Ill Defined Symptoms (No Diagnosis
|
3,912
|
4.83
|
6.
|
Anemia-Mild & Severe
|
9,944
|
4.07
|
7.
|
Intestinal Worms
|
3,135
|
3.87
|
7.
|
Diabetes Mellitus
|
8,285
|
3.39
|
8.
|
Other Non-Infectious GIT Diseases |
3,052
|
3.77
|
8.
|
Rheumatoid and Joint Diseases
|
7,502
|
3.07
|
9.
|
Skin Infection - Fungal
|
2,517
|
3.11
|
9.
|
Skin Infection-Fungal
|
5,687
|
2.33
|
10.
|
Anaemia, Severe & Mild/Moderate
|
2,129
|
2.63
|
10.
|
Intestinal Worms
|
5,359
|
2.19
|
HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
Halmashauri ya manispaa ya morogoro ina jumla ya vituo 58 vinavyotoa huduma za afya ya uzazi,24 (40%) kati ya hivi vinatoa huduma ya kujifungua na vituo 5 vinavyotoa huduma jumuishi za kujifungua na dharura za uzazi.Katika kipindi cha mwaka 2023
N.B Halmashauri imeweka lengo la kushusha vifo kwa asilimia 50% kwa kipindi cha miezi 6.
HUDUMA ZA CHANJO
Huduma za chanjo zimeendelea kutolewa kwa walengwa ambao ni watoto walio katika umri wa kupata chanjo, wasichana wenye umri wa miaka 14, wanawake walio katika umri wa kujifungua na walengwa wengine kwa makundi yao kulingana na aina ya chanjo wanazostahili.
Kampeni mbalimbali zimetolewa ikiwa ni Pamoja na utoaji jumishi wa chanjo ya Mlango wa kizazi na chanjo za nyongeza kama jedwali linavyojionesha hapa chini.
IDADI YA WATU WALIOCHANJWA:
NA
|
AINA YA CHANJO
|
MALENGO
|
WALIOCHANJWA
|
KIWANGO CHA UCHANJAJI
|
1 |
CHANJO DHIDI YA KIFUA KIKUU
|
12,713 |
23,402 |
184% |
2 |
POLIO
|
12,713 |
20,262 |
159% |
3 |
POLIO YA SINDANO
|
11,522 |
14,578 |
127% |
4 |
CHANJO DHIDI YA PNEUMONIA
|
11,522 |
14,596 |
127% |
5 |
CHANJO DHIDI YA KUHARA
|
11,522 |
14,637 |
127% |
6 |
SURUA
|
11,522 |
15,001 |
130% |
7 |
DONDAKOO, PEPOPUNDA NA KIFADURO (DTP)
|
11,522 |
14,807 |
129% |
8 |
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (HPV)
|
4,855 |
6,001 |
124% |
9 |
PEPOPUNDA NA DONDAKOO KWA WAJAWAZITO
|
12,713 |
13,293 |
105% |
AFP 5 (133%) FRI 15(120%)
DAWA NA VIFAA TIBA
Hali ya upatikanaji wa dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa Halmashauri kwa mwaka 2023 ilikuwa kwa wastani wa asilimia 95.2% kulinganisha na 94% mwaka 2022 kwa mujibu wa mfumo wa eLMIS.
Dawa na vifaa tiba vilizokosekana katika baadhi ya vituo ni Pamoja na diclofenac inj , liginocaine inj , gauze ,Urine Pregnant test, unalysisi strips,gauze, examination gloves mzani wa watoto na microscope uhaba huo ni kutokana na kukosekana MSD
Tatizo ambalo lilitatuliwa kwa kuomba dawa na vifaa tiba hivyo toka kwa washitiri wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi nakupandisha upatikanaji wa dawa na vitendanishi kufikia wastani wa asilimia 98%
UAGIZAJI WA DAWA, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI MSD NA KWA MZABUNI TEULE
Bidhaa zenye thamani ya Tsh. 758,194,978.68 zimepokelewa katika Halmashauri kwa kwa kipindi cha julai 2023 mpaka machi 2024 kwa mchanganuo ufuatao, mwaka 2023 Tsh. 765,585,547.00 zilipokelewa kwa ajili ya Dawa na vitendanishi toka MSD na Tsh. 117,287,149.88 ni mfumo jazia toka kwa Wazabuni teule, ilikujazia dawa na vitendanishi vilivyokosekana bohari ya dawa (MSD)
KIPINDI
|
THAMANI MAPOKEZI MSD
|
THAMANI MAPOKEZI WASHITIRI
|
JULAI-SEPTEMBA
|
192,372,256.39
|
60,899,099.19
|
OCTOBA-DESEMBA
|
296,792,176.80
|
31,165,555.00
|
JAN-MARCH 2024
|
151,743,395.61
|
25,222,495.69
|
JUMLA YA FEDHA
|
640,907,828.80
|
117,287,149.88
|
Aidha baadhi ya vifaa tiba vilipokelewa katika vituo vya kutolea huduma ambavyo ni
X-ray machine, hospital bed, wheelchair, bed sheet, oxygen concentrator, examination bed, delivery beds
Ultrasound machine, Dental chair zenye dental X-ray, mayo table, mahine ya usingizi na vifaa vya upasuaji, infant radiant warmer, blood warmer, patient monitor , delivery set
TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA ZA RUZUKU TSH. 600,000,000 KWA AJILI YA UNUNUZI WA VIFAA TIBA.
Kiasi tajwa hapo juu kilipokelewa kwa ajili ya ununuzi wa wa Vifaa Tiba. Mgawanyiko wa manunuzi ya vifaa umefanyika katika vituo nane vipya ambavyo ujenzi wake umekamilika na vifaa venye thamani ya Tsh. 200,000,000.00 (kwa mwaka 2022/2023) viliagizwa na fedha zake zililipwa katika akaunti za bohari kuu ya dawa (MSD) za vituo na Tayari Vifaa vyenye thamani ya Tsh. 161,505,949.29 toka Bohari vimepokelewa hii ikiwa ni asilimia 80.8 ya mapokezi
Aidha Halmashauri ilipokea fedha za Vifaa Tiba (2023/2024) toka serikali kuu kiasi cha Tsh 400,000,000.00 ambapo manunuzi ya vifaa yamefanyika na kupokea baadhi ya vifaa Tiba vyenye thamani ya Tsh 196,039,949.72 ambayo ni asilimia 49 ya vifaa vilivyopokelewa na malipo yake yamekamilika.
MAOTEO
Halmashauri ilifanya maoteo ya bidhaa za Afya mnamo Mwezi Agosti 2023 yenye thamani ya Tsh 1,955,857,518.00 kwa vituo 38: ikiwa ni Hospitali tatu (3) , Vituo vya Afya sita (6) na zahanati ishirini na tisa (29)
IDADI YA VITUO
|
JINA LA KITUO
|
THAMANI YA MAOTEO
|
3
|
HOSPITALS
|
621,061,736.00
|
6
|
HEALTH FACILITIES
|
507,550,134.00
|
29
|
DISPENSARIES
|
827,245,648.00
|
TOTAL FACILITIES 38
|
TOTAL AMOUNT
|
1,955,857,518.00
|
HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII
Huduma za Ustawi wa Jamii hutolewa kwa kufuata Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.Maeneo yanayosimamiwa na kitengo cha ustawi wa jamii ni pamoja na:
Huduma ya Ustawi wa Jamii wa Familia na Watoto
Huduma ya Marekebisho ya Tabia na Haki za Mtoto Kisheria
Huduma kwa Wazee na Watu Wenye Ulemavu
IDADI YA VITUO VYA KULELEA WATOTO WADOGO MCHANA (DCC) NA MAKAO YA WATOTO YATIMA
AINA YA KITUO |
IDADI |
YALIYOSAJILIWA |
VISIVYOSAJILIWA |
VITUO (DCC)
|
103
|
42
|
61
|
MAKAO
|
12
|
11
|
1
|
NYUMBA SALAMA
|
3
|
0
|
3
|
Mkakati
Ni kuendelea kuvifanyia ukaguzi vituo vile ambavyo vina hali nzuri visajiliwe na vile vinaonekana hali yake ni mbaya haviwezi kusajiliwa kulingana na mwongozo uliopo ni kuvifunga.
HALI YA UKATILI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO
Aina ya Ukatili
|
Watu wazima
|
Jumla
|
Watoto |
|||
Me |
Ke |
Me |
Ke |
Jumla
|
||
Ukatili wa Kimwili (vipigo)
|
02 |
15 |
17 |
11 |
22 |
33 |
Kingono (kubakwa/Kulawitiwa)
|
0 |
10 |
10 |
25 |
67 |
92 |
Ukatili wa Kihisia
|
03 |
14 |
17 |
27 |
93 |
120 |
Wahanga walioripoti ndani ya masaa 72 baada ya tukio
|
0 |
0 |
0 |
7 |
9 |
16 |
Wahanga waliopata matibabu ya Kinga(PEP)
|
0 |
0 |
0 |
7 |
9 |
16 |
JUMLA KUU
|
5 |
39 |
44 |
77 |
200 |
277 |
UTEKELEZAJI WA KUPUNGUZA MATUKIO YA UKATILI
UUNDWAJI WA MABARAZA YA WAZEE, KAMATI ZA WATU WENYE ULEMAVU NA KAMATI ZA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO
ENEO |
MABARAZA YALIYOUNDWA NGAZI YA HALMASHAURI |
IDADI YA KATA ZILIZOPO |
KATA ZILIZOUNDA |
MITAA ILIYOPO |
MITAA ILIYOUNDA |
MABARAZA YA WAZEE
|
1 |
29 |
29 |
294
|
294
|
KAMATI ZA WATU WENYE ULEMAVU
|
1 |
- |
- |
294 |
294 |
KAMATI ZA MTAKUWWA
|
1 |
29 |
29 |
294 |
294 |
VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO
Idadi ya watoto chini ya miaka mitano walioandikishwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa ni watoto 8890 amabapo watoto wa kiume ni 3,720 na watoto wa kike 5,170. Vyeti vilivyoingizwa kwenye mfumo ni vyeti 5,678 sawa na asilimia 63.8%, hii ni kutokana na changamoto ya ubovu wa simu za kusajilia vyeti vya kuzaliwa.
MIKAKATI KWA AJILI YA USAJILI
HUDUMA ZA LISHE.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imeendelea kuboresha utekelezaji wa Afua za lishe kwa kuzingatia ubora wa huduma katika vituo vya kutolea huduma na ueimamizi wa mkatbata wa viashiria vya lishe
HALI YA LISHE
|
IDADI
|
ASILIMIA
|
UDUMAVU
|
208/6940
|
3%
|
UZITO PUNGUFU(NEWBORN)
|
1467/1944
|
7.5%
|
UPUNGUFUWA DAMU(WANAWAKE WAJAWAZITO
|
343/17143
|
2%
|
UZITO ULIOZIDI(WATOTO)
|
110/7434
|
1.5%
|
Utekelezwaji wa Afua za lishe umeendelea kuzingatiwa kwenye usimamizi wa viashiria vya Mkataba wa lishe Pamoja na huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya. Halmashauri ina jumla ya watoto 49,575 waliochini ya miaka mitano
Katika kipindi cha mwaka 2023/24 halmashauri imezingatia muongozo wa utengaji wa fedha za lishe na kutenge sh 1334 kwa kila mtoto na kufanya jumla sh (66,133,050mapato ya ndani) kwa ajili ya matumizi ya utekelzaji Afua za lishe .
Pia shilingi 7,642,000/=zimetengwa kutoka mfuko wa pamoja yaan(busket fund)ambazo zimetengwa na kutumika kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na sh 3,170,000/=kutoka vyanzo vingine yaan(userfee,nhif, na ichf)
Na kufanya jumla ya fedha zote za utekelezaji wa Afua za lishe kuwa sh
76,945,050/=
MCHANGANUO WA UTENGAJI FEDHA ZA LISHE
NO
|
CHANZO
|
KIASI CHA FEDHA
|
1
|
MAPATO YA NDANI
|
66,133,050
|
2
|
BUSKET FUND
|
7,642,000
|
3
|
USERFEE
|
1,520,000
|
4
|
NHIF
|
800,000
|
5
|
Ichf
|
850,000
|
|
JUMLA
|
76,945,050/=
|
Jedwali likionyesha mchanganuo wa utengaji fedha za lishe kwa mwaka wa fedha 2023/24
Pia halmashauri imefanikiwa kuwajengea uwezo watendaji wa mitaa 147, na wahudumu ngazi ya jamii 167.Lengo ni kuendelea na kuimarisha utekelezaji wa Afua za lishe ngazi ya mitaa na kaya kwa ujumla.
Sambamba na hilo Halmashauri imefanikiwa kununua length board 29 kutumia mapato ya ndani na pia kuzigawa kwenye vituo vya kutolea huduma
huduma za lishe zimeendelea kutolewa katika vituo vya kutolea huduma na watoa huduma 63 wamejengewa uwezo juu ya utambuzi wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kutumia vibao (lengh board) Pamoja na maswala mengine ya usimamizi wa viashiria vya lishe ngazi za vituo.
BIMA YA AFYA YA JAMII ILIYOBORESHWA (iCHF)
Kiwango cha uandikishaji wa wateja wa ichf kuanzia mwezi julai 2023 hadi kufikia machi 2024 ni kaya 1313 zenye wanufaika 6801.Aidha vituo viliweza kupokea marejesho kwa kipindi tajwa ya jumla ya kiasi cha Tsh 19,441,964.92.
CHANGAMOTO KUBWA ZA JUMLA
MIKAKATI NA UTATUZI
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa