VIVUTIO VYA UTALII NDANI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO
UTANGULIZI
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ndio makao makuu ya mkoa yalipo. Ni mojawapo ya miji mikongwe katika historia ya Tanzania [ikiitwa Tanganyika] katika karne ya 18. Waarabu walitumia Morogoro kama kituo chao cha kupumzikia wakati wa biashara ya utumwa na kabla ya kuwapeleka mashariki ya mbali kwa ajili ya kuwauza kupitia Bandari ya Dar es salaam katika bahari ya Hindi.
Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali. Kabila ambalo ni wenyeji wa Halmashauri hii ni Waluguru. Morogoro ilipanda kufikia hadhi ya kuwa mji mwaka 1962. Kasi ya kupanuka kwa Halmashauri ya mji iliongezeka kidogo kidogo na ilipofika tarehe 1/7/1988 ikapanda hadhi na kuwa Manispaa. Kutokana na fursa mbalimbali zilizopo kijiografia, kiuchumi na kimazingira, jitihada zinafanyika kupitia Halmashauri na Wadau mbalimbali kuendeleza Manispaa katika nyanja mbalimbali ili kufikia hadhi ya Jiji siku za usoni.
Manispaa ya Morogoro iko umbali wa Kilometa 195 kutoka Jiji la Dar es Salaam. Ipo kati ya Latitudo 4.5 Kusini na Longitudo 37.4 Mashariki. Ipo kiasi cha futi 1,600 kutoka usawa wa bahari. Manispaa inapakana na milima ya Uluguru kwa upande wa Kusini na Milima ya Mindu kwa upande wa Magharibi. Upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya ya Mvomero na Morogoro kwa upande wa Mashariki.
Lakini pia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inavyo vivutio vingi vya utalii vya aina mbalimbali hasa mimea na ndege wa aina mbalimbali katika ukanda wa kusini (Southern Tourist Circult).
VIVUTIO VINAVYO VAPATIKANA HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO
Hifadhi ina ukubwa wa kilomita za mraba 1,990; ni hifadhi yenye viumbe ambavyo havipatikani maeneo mengine kokote duniani: Mbega wekundu (Iringa red colobus) na Sanje crested mangabey; ndege: chozi bawa jekundu (Rufous-winged sunbird) na jamii mpya Kwale kugunduliwa (Patridge-like Francolin).
Maporomoko ya maji Kibwe, maporomoko ya maji choma (Chalagule) na Maporomoko ya maji ya Hululu yakianguka na kutua mithili ya ukungu.
Aina ya maua adimu: African violet
Mlima huu ni mlima wenye uoto wa asili na theluji, Kupanda na kufikia kilele chake kunakupatia muonekano na mandhari ya kipekee na sababu za hisia zisizo hesabika kwa kuwa juu Mji mzima wa Morogoro na Mkoa mzima ukiwa umelala chini ya miguu yako.
Safu za Milima ya Uluguru: Safu hizi ziko Kusini Mashariki mwa Morogoro ukitembelea utapata nafasi ya kujifunza kuhusu historia ya makabila ya asili, Mazao mbalimbali, Wanyama pori na vyanzo vya Maji ambavyo vinatengeneza Mto Ruvu ambao hutumika kupeleka Maji Mji wa Dar es salaam.
VIVUTIO
Mlima huu ndio mlima mrefu na uliosambaa kuliko yote ndani ya Mkoa wa Morogoro uliosimama na kusambaa kwa kujitegemea. Mlima huu una umaarufu mkubwa ndani nanje ya Mkoa wa Morogoro kutokana na historia yake kutokana na mandhari ya kipekee ya hifadhi ya mlima uluguru ambao una jumla ya Vilele Zaidi ya vine ambavyo ni Uwanda wa Lukwangule (Lukwangule plateau) ambao uko meta 2638 kutoka usawa wa bahari, Lupanga ambacho kipo meta 2138 kutoka usawa wa bahari, Kimhandu ambacho kipo meta 2636 kutoka usawa wa bahari, na Kilele cha Bondwa ambacho nacho kipo meta 1220 kutoka usawa wa bahari.
Kilele cha Bondwa: Ni moja ya Maeneo ya kihistoria na Kitalii na ni sehemu nzuri sana ya kufurahia iko umbali wa Km 6.3 kutoka Morogoro Mjini, umbali wa muda wa Saa Tano ivi kwa kutembea.
Ni kilele kinachofikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa vutia Watalii wengi kutoka pande zote za dunia hasa wale wanaobahatika kutembelea hifadhi hii. Vivutio vingine katika hifadhi hii ni pamoja na baadhi ya Vinyonga wenye pembe tatu ambao wanapatikana katika milima hii pekee: hawapatikani mahali pengine popote, Mimea adimu-135, Ndege wa pekee anayeitwa Wami-mbizi, Ndege (Ulugruru Violet-backed sunbird, Maporomoko (Hululu and Kibwe falls), Mapango, NJia asili ya Tegetero ambapo unaweza kuona muonekano mzuri ‘landscape’ wa safu za milima ya uluguru(Tegetero trails), Morning site, Bunduki Corridor na Bondwa peak na Mimea ambayo ni adimu na pekee-Africam violet – Saintpaulia, Panzi mwenye rangi zote za bendera ya Taifa la Tanzania.
SHUGULI ZA KITALII
MALAZI
Kuna hoteli za kitalii, nyumba za kulala wageni zinazo faa kwa watanzania kambi za kupiga mahema na pia hosteli kwa ajili ya makundi maalumu kama wanafunzi.
NJE YA HIFADHI
Kuoona Mji wa Morogoro uliokaribu na hifadhi ambapo huko utapata aina mbalimbali za malazi.
NYAKATI NZURI ZA KUTEMBELEA HIFADHI
Ni wakati wa kiangazi kuanzia mwezi Juni – Agosti aidha, wakati wa masika mwezi Novemba hadi Machi (kwa ajili ya kuona mimea, maua na vipepeo) na Desemba hadi Fembruari (kwa kuwaona makundi ya ndege wahamiaji).
JINSI YA KUFIKA
Hifadhi hii inafikika kwa njia ya ndege nyakati zote. Kwa njia ya barabara inafikika kutokea Dar es salaam, Dododa na Kutokea Iringa hadi Morogoro Mjini. Zipo ndege za kukodi kutoka sehemu mbalimbali zitakazo kufikisha hadi Morogoro Mjini.
2. MAPANGO MLIMA WA MGURU WA NDEGE
Mapango haya yaliypo kwenye mlima wa mguru wa ndege yalitumika wakati wa vita ya kwanza na ya pili ya dunia, kuanzia mwaka 1914 - 1918 vita ya kwanza ya dunia mpaka mwaka wa 1939 – 1945 vita ya pili ya dunia. Pamoja na matumizi ya mapango hayo miaka hiyo pia mpaka sasa mapango haya yanatumika kwa ibada na mapumziko ‘picnic’ kwa watu mbalimbali ndani na nje ya nchi na hasa wale wanaokuja kwa ajili ya utalii au mapumziko.
3. MAENEO YA KIHISTORIA NA MALI KALE
Mnara wa Kumbukumbu wa Mashujaa: Mahali ulipo mnara huu upo kwenye mzunguko wa posta Morogoro Mjini, ni mnara wa kumbukumbu ya mashjaa waliopigana vita vya kwanza na vya pili vya Dunia na vita vya Kagera katika kuazimisha kumbukumbu za mashujaa waliopigana kwa kutumia zana za kale ikiwemo Mkuki, Mishale na Ngao.
Kambi ya wapigania uhuru wa Namibia na Zimbabwe: Mahali hapa; kambi hii iko eneo la nyuma ya Gereza la Mkoa na FFU kambi hii ilitumika na wapigania uhuru wa vyama vya SWAPO, ZANU-PF; SWAPO ni wapigania uhuru wa Namibia, ZAPU na ZANU-PF ni wapigania uhuru wa Zimbabwe. Kambi hii ilikuwa ni maalumu kutoa mafunzo kwa waganga wauguzi kwa sasa kambi hii inamilikiwa na Jeshi la Polisi kama Makazi.
Common Wealth Graves: Mahali yapo; karibu na Chuo cha Mifugo LITA haya ni Ishara ya Makaburi ya Wajerumani na Waingereza waliopigana vita vya kwanza na vya pili vya Dunia wakiamini hawatasahaulika kwa alama zilizowekwa.
Makaburi ya Mazimbu: Mahali yapo; Makaburi haya yako eneo la Kampas ya Chuo cha Kilimo cha Sokoine Mazimbu, makaburi haya ni ya wapigania Uhuru wa ANC (African National Congress) wa Afrika ya Kusini ambao walipoteza maisha katika matukio mbalimbali ikiwemo Ugonjwa, Ajali walioishi Morogoro Mjini. Pia inatambulika hii ni kambi ambayo ilitoa mafunzo mbalimbali ikiwemo Shule, Chuo kwa wapigania Uhuru hao. Kwa sasa inamilikiwa na Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kama chuo katika kutoa Elimu ya Juu.
Makanisa ya Kwanza ya Wakoloni: Kanisa moja lipo eneo la Chuo cha Ualimu Morogoro (Kigurunyembe) ni Kanisa la kwanza la Waroma ambalo lilitumika kwa ajili ya Ibada. Hadi sasa kanisa hilo linatumika na Waumini wa Roman Katholic. Pia Kanisa lingine lipo eneo la Shule ya Sekondari ya Kingurunyembe, kwa sasa Kanisa hili linatumika kama eneo la Kulala Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kigurunyembe.
Nyumba za Kale: Nyumba hizi ziko eneo la Mji Mpya, nyumba hizi zilikuwa zinatambulika kwa jina la (kwa Paju). Kwa sasa Nyumba hizo bado zinatumika kama Makazi ya Watu.
Morning Side: Iko kwenye Tao la Mashsariki, Milima ya Uluguru Kaskazin, iliyojengwa na Wajerumani Miaka ya 1900, Nyumba iko usawa wa Mita 900 usawa wa Mlima Uluguru ilikuwa ikitumika kwa ajili ya mapumziko. Jengo hili lilikuwa linatumiwa kama Hotel na Hostel ya Wajurumani lakini pia kuna Kanisa pembezoni ambalo lilikuwa likitumika kwa ajili ya Ibada ambalo mpaka sasa linatumika na wakazi wa eneo hilo.
Choma Water fall: haya ni Maporomoko ya Maji yaliyoko kwenye Kijij cha Choma, Maporomoko haya huungana na Maporomoko mengine madogo madogo na kutengeneza Mto Ruvu.
Bwawa la Mindu: Liko Km 9 Kusini Magharibi mwa Manispaa ya Morogoro likichukua eneo la Km za mraba Nne lilijengwa/kutengenezwa kwa lengo la kukidhi matumizi ya Maji Majumbani na Viwandani, hiki ni chanzo kikubwa cha Maji kinacho hudumia Zaidi ya Asilimia 80 ya wakazi wa Morogoro, Bwawa lina mandhari nzuri na viumbe hai mbalimbali wakiwemo Samaki na Ndege.
Lupanga peak: ni kilele kirefu Zaidi katika Safu za Milima ya Uluguru chenye urefu wa 2147m kilele hiki kimezungukwa na Misitu ya asili na aina mbalimbali za viumbe hai wakiwemo Ndege.
Gereza la kwanza la Watumwa: Gereza la kwanza la kwanza a watumwa – hapa ni mahali ambapo walikuwa wanatumia kuadhibia ambapo kulikuwa na Mti lilitumika kunyongea.
Mashamba ya Mkonge: ni ushahidi kuonesha kuwa Wageni walikuja na Mitazamo ya uzalishaji wa Mikonge na kupeleka kwao.
Boma – British Oversees Management and Admnistration: ni Majengo yaliyojengwa na Wageni kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za kiserikali mfano palipo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Makaburi ya Chief Kingo na Kisebengo: Makaburi haya yako nyuma ya Ofisi za Shirika la Nyumba na TBC Taifa, Makaburi hayo ndio ushahidi ya walipolala Viongozi wetu wa Kijadi na yamebaki kama sehemu ya kihistoria na kumbukumbu muhimu ya mila na desturi yetu/zetu hasa Waluguru. Aidha makaburi haya yamekuwa ni sehemu ya Vivutio vya Utalii katika Mkoa wetu wa Morogoro.
Mwembesongo: Songo alikuwa Mtu maarufu sana ambaye alikuwa akiishi karibu na Muembe, mti huo ulibeba jina lake na kuita Mwembesongo, kihistoria ambapo Wazee walikuwa wanakutana kwa ajili ya mazungumzo, Mwembe huu mpaka sasa upo na ndio chanzo cha Jina Mwembesongo.
Njia ya Utumwa: hii route inaanzia Bagamoyo mpaka Ujiji Kigoma na ilipitia hapa Manispaa ya Morogoro, kupita hapa ilikuwa lazima kulipa ushuru kwa Machifu wa hapa, hivyo kilikuwa ni chanzo cha mapato kwa viongozi wetu wa Jadi. Uwepo wa Mzambarau na Mikarafuu ilitokana na Chief kuzuia Mimea iliyokuwa ikipitishwa hapa hivyo walikuwa wakijatahidi kumdanganya Chief badala ya kummletea mimea ya Mikarafuu wakamletea Mizambarau, lakini baada ya muda mrefu kuikuza na kuona sio yenyewe Waarabu walibanwa na kuleta Mikarafuu.
VIVUTIO
SHUGULI ZA KITALII
Utalii wa kutembea kwa miguu
Utalii wa kuogelea
Utalii wa kutumia magari
Utalii wa kupiga picha
Utalii wa kuona
Kutembelea maeneo ya kihistoria ya biashara ya watumwa.
Utalii wa kiutamaduni (cultural and historical sites) ndani na nje ya hifadhi
MALAZI
Utakapo ingia katika Mji wa Morogoro ambako kivutio hiki kinapatikana utapata malazi ndani na nje ya vyanzo hivi vya hifadhi ambavyo ni:Kuna hoteli za kitalii, nyumba za kulala wageni zinazo faa kwa watanzania kambi za kupiga mahema.
NJE YA HIFADHI
Nyumba za wageni kambi za kudumu za mahema
4. BUSTANI YA MAWE (Rock Garden Resort Tour)
Ipo Kilometa 2 Mashariki kutoka Morogoro Mjini kwenye Mlima pembeni kabisa ya Mto, sehemu hii ni ya asili hivyo ni kivutio kizuri kwa Watalii wa Ndani na Nje, ina Maporomoko ya Maji yanayotiririka mwaka mzima yanayopita kwenye Mawe makubwa yenye Mabwawa ya asili ya kuogolea, kuna Ndege, Wanyamapori wadogo wadogo kama Ngedere, Pimbi na Jamii ya Mijusi na Misitu ya asili kama vile Mikangazi pori. Aidha pia hapo kunapatikana vyakula na vinywaji vya aina zote, ni sehemu nzuri ya kupiga Mahema, Kuogelea na Kufurahi mandhari nzuri ya asili na viumbe vyake.
SHUGULI ZA KITALII
5. TAMADUNI, DESTURI NA MILA
HISTORIA YA WALUGURU
Asili ya neno Morogoro ni Mluguru ili kujua zaidi twende pamoja.
KAMA utairejea historia ya Morogoro ya miaka ya kati ya 1870 hadi 1888, kipindi ambacho Sultan wa Zanzibar alikuwa Sayyed Barghash, utagundua kuwa kwenye safu ya Milima ya Uluguru na pembezoni mwake kulikuwa chini ya Machifu wa makabila tofauti ambayo leo hii yanaitwa “Koo za Kiluguru”.
Makabila na koo zilizokuwepo hadi mwaka 1888 kote Uluguruni yakizungumza lugha inayofanana na kufuata mila zinazorandana ni pamoja na Wabena, Wamwenda, Walelengwe, Wabunga, Wacheti, Wachaga, Wagweno, Wabinga, Wachiru, Wachuma, na Wagonanzi.
Wengine ni Wahafigwa, Wahimba, Wamwingu (Waingu), Wakibago, Wakiflagu (ambao ni wachache sana Uluguruni), Wakinoge, Wakiraru, Wakuruwa, Wakonga, Wakumburu, Wakwama, Walari, Wamanga, Wamasenga, Wamangara, na Wamaze.
Pia walikuwepo Wambiki (Wangode), Wambonde, Wambega (Wakiru), Wanyani (Wanyagatwa), Wamlali, Wamugera, Wamwandike, Wanambo, Wangandi, Wangozi, Wangurumi, Wangweku, Wanyanga, Wanzovu na Waponera.
Halikadhalika walikuwepo Wasikoni, Wasinogi, Watebe, Watemaruge, Watonga, Wanzangazwa, Wazeru, Wazima na Wazongo.
Baadhi ya haya yalikuwa ni makabila, na nyingine ni koo zilizotokana na makabila yaliyokuwepo Uluguruni au nje ya hapo.
Utafiti unaonesha kuwa, zipo baadhi ya koo hazikutokana kabisa na makabila ya kibantu, yaani baadhi zilitokana na Wafilipino waliyoko Asia kusini, na wengine walitokana na makabila ya kiarabu.
Pia wapo waliotokana na Wazulu waliotoka moja kwa moja Afrika Kusini, au wale waliotangulia kabla kukwepa vita ya Chaka Zulu wakiwemo Wanyasa, Wamanda, Wangoni, Wabena na wengineo ambao majina yao yalibadilika kutokana na maeneo waliyoishi, au matukio waliyokutana nayo.
Wapo pia waliotokana na makabila ya bara ikiwemo Wanyamwezi, na makabila ya kaskazini ikiwemo Kilimanjaro, milima ya Upare, na Unguu na kadhalika.
Makabila au koo zote hizi kwa bahati zilizungumza lugha moja na kufanana kitamaduni japo baadhi ya mila na desturi zao zilitofautiana kutegemea na asili zao.
Ufananaji wa Lugha ulitokana na Lugha ya wenyeji wa mwanzo kutangulia kufika na kuweka maskani katika safu ya milima hii, ambao ni Wamwenda, wengi wao kwa sasa wanapatikana Tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero, kusini maghalibi ya Milima ya Uluguru.
Hivyo wengine waliofuatia walijitahidi kufahamiana na wenyeji na kulazimika kujifunza lugha na utamaduni wao, japo baadhi ya mambo ya msingi wametofautiana hadi leo.
Lipo swali linaloulizwa nini hasa asili ya neno Luguru, na neno Morogoro, Hilo ni somo la peke yake linalohitaji muda mrefu kulijadili, cha msingi hapa kuzingatia kuwa Uluguru hapo kabla lilikuwa ni eneo na si kabila, isipokuwa wale wote walioishi katika eneo hili na pembezoni mwake Wajerumani waliwajumuisha katika kundi moja na kuwaita kuwa Waluguru.
Machifu wa Kiluguru wakati huo walimkubali muwindaji mahiri mwenye asili ya Uzigua Bwana Kisebengo kuwa Kingo (Kinga) yao katika uwanda wa chini, na kumruhusu ajenge mji wake.
Pia zipo simulizi zingine zinasema kuwa asili ya neno Luguru ni kuwa miaka ya 1800 kundi la watu walikuwa wakisafiri kutoka kusini mwa Morogoro ya sasa kuelekea mashariki yaani Bandari ya Salama, wakiwa katika msafara wao kiongozi wao aliamua kupanda katika milima inayoonekana hapo Morogoro ya sasa. Alikaa sana huko mlimani bila kurejea, hivyo wakaamua kumfuatilia na bahati mbaya wakakuta ameliwa na wanyama na kubaki mguu mmoja tu. Kwa heshima wakachukua mguu ule na kuamua kurudi chini huku wakiomboleza, na kila watu walipowaona walisema wale wa LUGURU – yaani wale waliobeba mguu.
Asili ya neno Morogoro inatokana na neno Mluguru, hii ni kuwa mjerumani alishindwa kutamka neno mluguru hivyo akatamka MOROGORO (yaani hapa sauti ikiwa inatoka katika koo sio kutoka katika ulimi, waweza kujaribu pia). Kutoka hapo mjii huo ukaitwa Morogoro.
‘Kingo’ Kisebengo alijenga mji mdogo katika njia ya Kaskazini ya milima ya Uluguru inayounganisha Pwani ya Afrika mashariki na bara, jirani na mji wa sasa wa Morogoro ambao wakati huo ulikuwa msitu.
Machifu wa Kiluguru walikubaliana na Kisebengo kuwatoza ushuru wale wote wanaotumia njia hiyo kwa ajili ya safari zao za kibiashara, kutokana na ukweli kuwa Wananchi wao ndiyo walioijenga, na kuendelea kuilinda na kuitunza njia hiyo muhimu.
Baadhi ya wafanyabiashara walikubali na kulipa, ila wengine waligoma, ingawa hawakuwa na ubavu wa kupambana kivita na Kisebengo wala waandamizi wake wa Kiluguru, hivyo wakahiyari kutumia njia ya kusini, iliyoko baina ya upande wa kusini wa milima ya Uluguru na bonde la mto Rufiji.
Njia hii pia ilielezwa kupitishia watumwa, jambo ambalo linapingwa na machifu wa wakati huo Lukwele wa Choma aliyezaliwa mwaka mwaka 1852 na kufariki mwaka 1971, akizikwa makaburi ya Kichangani mjini Morogoro.
Chifu Lukwele ndiyo yule wakati fulani aliyekuwa askari aliyepigana katika jeshi la Mjerumani dhidi ya Waingereza na washirika wao, kwenye maeneo kadhaa ya Mashariki ya Kati (bara Arabu), Afrika Mashariki, Msumbiji, Malawi na hatimaye Namibia, na kurejea nchini baada ya vita ya kwanza ya Dunia kumalizika katika muongo wa pili wa karne ya 20.
Lukwele ambaye jina lake halisi ni Salum bin Msumi, alikuwa ni mmoja kati ya watoto watatu mashuhuri wa Chifu Msumi wa Kibungo, ambaye asili yake kwa baba na mama ni Mzulu toka Afrika Kusini.
Hivyo wafanyabishara wa Utumwa hawakuthubutu kupita eneo hilo, bali walipita njia ya kusini.
Wamishenari, Wavumbuzi na wapelelezi wa mwanzo, waliofanya safari za bara au pwani mara kwa mara, baadhi yao walipita njia hii muhimu katika karne hiyo ya 19.
Mmoja kati ya hao ambaye Historia ya Waluguru imemrekodi na kumkariri sana ni Keith Johnson ambaye alishazungukia eneo la Maasai, na Ziwa Victoria, kisha kupita njia hii akielekea pwani.
Alipoingia katika eneo la Waruguru na Wakutu, Jasusi huyo bobezi akielekea ukanda wa kati na Maziwa makuu mwaka 1879, kwa mara ya kwanza alishangazwa na umbile la ajabu la sehemu ya tao hili la milima ya Mashariki ya Afrika.
Hata kabla ya kusafisha mboni zake za macho kuona madhari asilia ya kuvutia na kuweka historia, roho yake ikaacha mwili, alipofariki eneo la Ukutu mwaka huo, na kuzikwa Behobeho kusini ya Kisaki.
Msaidizi wake mkuu Joseph Thomson wakati huo akiwa ni kijana mbichi asiye na uzowefu mkubwa, akitimu umri wa miaka 23 tu toka kuzaliwa kwake, akabeba mikoba ya mtangulizi wake.
Thomson kama ilivyo kwa mwandamizi wake alivutiwa mno na safu hii ya milima adhimu ya Uluguru kiasi cha kushika kalamu katika moja ya maandiko yake akiweka bayana kuwa; “Uwasili umemwaga utajiri wa maliasili zake, na kuzalisha kila kinachoweza kutuliza moyo na mwili, halkadhalika kuburudisha macho kwenye tao la milima hii”.
Thomson anaweka wazi kwamba, katika njia ya chini hakubahatika kuwaona Waluguru zaidi ya kupata habari zao toka kwa wanajeshi wa kabila la Wambunga, waliojaribu bila mafanikio kuvamia milimani kwa njia ya vita, kupora vyakula kutokana na ‘nchi’ zao kuwa na njaa kali.
Wambunga walimwambia kuwa, Waluguru walikuwa na majeshi imara yaliyojua sana kutumia vita ya upanga na kiasi mishale, hivyo kwa jiografia yao tata ya milimani, na uwezo wao wa kijeshi ilikuwa vigumu sana kuwafikia, japo walijaribu kufanya hivyo baadhi ya nyakati.
Aliambiwa na Wambunga pia kuwa, Waruguru hawakuwa na nguo, bali walivaa majani ya migomba, jambo ambalo baadaye alikuja kufahamu kuwa si la kweli! Rejea: (Kitabu cha Joseph Thomson: ‘To The Central Africa Lakes and Back’ cha mwaka 1881, I, Chapter 5).
Thomson alifahamu baadaye kuwa wanajeshi wa Kiluguru ndiyo waliovaa majani ya migomba na miti mingine kwa ajili ya kujificha dhidi ya adui katika uwanja wa mapigano, ilhali raia wa kawaida walivaa mavazi ya kujistiri kwa wanawake hasa Kaniki, na Marekani kwa mtindo wa kujifunga chini na kujitanda juu.
Na wanaume, pia walivaa kaniki kwa mtindo wa kujifunga kiunoni na juu lubega na pengine kujivika migolole hasa kwenye uwanda wa juu palipokuwa na baridi kali enzi hizo.
Aliwakuta Waluguru wakijali sana mila zao za asili kama vile unyago, ndoa, na kumbukumbu za watangulizi wao (matambiko).
Jasusi mashuhuri Henry Stanley naye alipita njia ya Kaskazini ya Tao la milima ya Mashariki hususan Uluguru, katika safari yake ya kumsaka “mvumbuzi” Dr. Livingstone na kulala katika ‘mji’ wa Simbamweni (mtoto mkubwa wa Kingo kisebengo), uliozungushiwa ukuta na kuwa na ngome isiyopenyeka kiurahisi (ambapo hivi sasa ni nje kidogo ya mji wa Morogoro wakati huo pakiwa msitu mnene na nyumba chache).
Stanley anausifu mji huo mdogo (Morogoro ya mwanzo kabisa) akisema kwamba umejengwa kwa mitindo ya kiarabu chini ya bonde la kijani la milima ya Uluguru, yenye misitu minene inayofunikwa na mawingu wakati wote wa mwaka, linalopambwa na mito miwili mikubwa na utitiri wa mifereji na vijito vya maji safi na salama, mandhari ambayo hajapata kuyaona katika eneo lolote alilowahi kufika katika Afrika Mashariki.
Henry Stanley anakisia kuwa Mji wa Simbamweni (Morogoro ya wakati huo) ukiwa na milango iliyotengenezwa kwa miti ya mitiki isiyozidi minne, yenye umbo la mraba kwenye ngome yake, ikifungwa wakati wote ila kwa hitajio, ulikuwa na wakaazi wasiozidi 3,000.
Anasema kwa mtazamo wake huwenda milango hiyo imara ya kuingilia mjini yenye maandishi ya Kiarabu ilitengenezwa Zanzibar au pwani na kupelekwa Morogoro kwa Simbamweni vipande vipande, kabla ya kuunganishwa (kutokana na ukubwa wake isingeweza kubebeka)!
Anakiri kuwa Morogoro ilibeba utajiri wa ajabu wa maliasili, Mazingira, maji na rasilimali watu, pamoja na ustaarabu wa hali ya juu, ambao hajapata kuuona ila katika nchi zilizoendelea wakati huo.
Mji wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro una tamaduni, mila na desturi za wenyeji kama vile maonyesho ya mapishi, ngoma za asili, ususi, ufinyanzi, mavazi na aina zake, mapishi ya aina mbalimbali, mfano kama vile; Matembezi ya Maasai Boma hili ni kabila dogo lakini na utamaduni wao ambao mara nyingi huwa vutia watalii wengi kutoka nje kuja kuwaona na kupata habari za kuvutia kutoka kwa kabila la wamasaai pia na kuona nyumba zao wanazo ishi huku wakiendesha shuguli zao za kila siku.
Utajionea Utamaduni wa kijiji cha Choma 1200m; utajionea maisha ya kabila la Waluguru jinsi wanavyo ishi na kuendesha maisha yao ya kila siku, hasa ngoma zao za kitamaduni utaburudika kula vya kula vyao vya asili(Mkembe – Ugali wa muhogo, Beze – majani ya magimbi, Togwa) na kuburudika kwa kujionea maisha yao ya asili.
VIVUTIO
SHUGULI ZA KITALII
Utalii wa kutembea kwa miguu
Utalii wa kupiga picha
Utalii wa kuona
Kutembelea maeneo ya kihistoria ya biashara ya watumwa.
Utalii wa kiutamaduni (cultural and historical sites) ndani na nje ya hifadhi
CHANGAMOTO ZA UTALII HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO
USHAURI
NJIA ZA KUKUZA NA KUENDELEZA SHUGULI ZA UTALII
Utalii huu wa ndani, unahitaji kukuzwa na kuendelezwa kwa kuongeza nguvu na ubunifu kwa njia kama hizi:
VIVUTIO VYA KITALII-
Hawa ni waanzilishi wa Mji wa Morogoro, makaburi yao yapo nyuma ya kanisa kuu la Roman catholic.
Mapango haya yanapatikana katika Milima iliyopo katika Msitu wa hifadhi wa Nguru ya Ndege kata ya Mkundi na Lukobe, watu wengi hutembelea Mapango hayo kwa ajili ya Kusali, Kutambika na Mapumziko siku za mwisho wa Juma. Kuna Misitu mizito yenye aina mbalimbali ya miti ya asili, Ndege na Wanyamapori, aidha ndiyo chanzo kikuu cha Mto Mkundi.
Hii ni Njia ya Miguu inaanzia Mtaa wa Misongeni kupitia Mtaa wa Vituli Kata ya Bigwa, inapatikana katika Misitu mizito ya milima ya Uluguru hadi Tegetero Mission ambako ni umbali wa kilmeta 8 toka Morogoro Mjini, huko kuna Ndege adimu waitwao African Violet na Uluguru bush-shrike (Allanblackia uluguruensis na Saintpaulia species) Ndege hawa huwezi kuwapata sehemu nyingine yoyote Dunian isipokuwa katika Milima ya Uluguru. Njia hii pia ilitumiwa na Chief wa Waluguru (Kingalu) na Wafuasi wake kwa ajili ya kufanya Matambiko kwenye Msitu wa Nguru iliyopo Wilaya ya Mvomero.
Ipo karibu sana na Mji wa Morogoro kupitia ‘’Morning Side’’ (6.3 Km kutoka katikati ya Mji wa Morogoro), utatembea katika hifadhi ya asili hadi kilele cha Bondwa ambapo ni Masaa 5 kwenda na kurudi. Ukiwa katika kilele cha Bondwa utaweza kuona Mandhari nzuri sana ya Mji wa Morogoro.
Hii ni Njia inayopitia Viwanja vya Tofari, katika Njia hii Watalii wataona aina mbalimbali za Miti ya asili, Ndege na Wanyamapori wadogo wadogo, Mijusi na Watalii huweza kufurahia hali ya hewa ya baridi ndani ya Misitu.
Utafurahia kutembelea eneo hili ambapo utakutana na Mbega Weusi na Weupe (Black & White Colobus Monkeys) huku ukifurahia Nyuso zao zenye aibu muda wote bila kumsahau Tumbili (Valvet monkey), kutembea kando ya Mto Kigurunyembe, kuogelea katika Mto (Usiingie ndani ya Mto). Utatizama Vivutio vyote hivyo ukiwa juu ya Vijilima vilivyopo katika eneo hili.
Kilele hiki kipo Uluguru kaskazini – mashariki – kusin mwa Mji wa Morogoro. Kilele hiki kina Mwinuko wa Mita 2138 kutoka usawa wa Bahari kwa njia ya Miguu na mwendo wa Masaa 6 – 10 hadi kileleni. Njia hiyo ina Miinuko ambayo huanzia mwa barabara ya Misitu iliyopo Mtaa wa Kibwe, hupitia Mashambani hadi kufikia hifadhi ya asili ya Uluguru hadi kileleni. Kupanda Mlima ni hatari sana kipindi cha Mvua hivyo unashauriwa kuwa na mwongoza wageni mzoefu. Wakati wa kupanda utaweza kuwaona Ndege kama vile Livingston turaco, Silvery checked hornabills na wengineo.
Nugh’utu iko 2.9Km na Kijiji cha Madolla ni 3.9Km kutoka Morogoro Mjini. Njia hii ina urefu wa Kilometa 2.5Km kwa Gari hadi Nugh’utu. Ukiwa Kijijini utajifunza jinsi Wanawake wanavyotengeneza Mikeka ya Udongo, pia utaona na kujifunza jinsi vyakula vya Jadi vinavyotayarishwa na utamalizia Safari yako kwa kutazama Ngoma za Jadi za wakazi wa maeneo hayo.
Kijiji cha Kinole ni maarufu sana kwa kuwa ndipo yalipo kuwa Makao makuu ya Mtemi wa 14 wa Waluguru. Kijiji hiki kipo Km 17.8 kutoka Morogoro Mjini mashariki mwa Milima ya Uluguru. Utapitia eneo la asilia la Nyayiko ambalo Mtemi Kingalu alilitumia kupumzika awapo Njiani kuelekea Mlima Nguru kwa ajili ya Matambiko na Kuabudu.
Maporomoko haya ya Maji yapo umbali wa Kilometa 53.3 kusin – mashariki mwa Mji wa Morogoro katika Kijiji cha Vinile, Kata ya Bunduki (Mvumero). Safari huanzia Morogoro Mjini, ni mwendo wa Nusu saa hadi kufika Mto Mgeta wenye Misitu mizito yenye Mijusi wengi, Vinyonga wenye Pembe moja na wengine pembe mbili. Mimea ya asili iliyopo ni pamoja na Allanblackia uluguruensis na Saintpauliagoetzeana. Ukiwa njiani ya kupumzikia Wageni, hapa kuna eneo kubwa la kuweka Nahema kwa gharama nafuu kabisa.
Safu ya Lukwangule ipo upande wa kusini mwa Uluguru, kilomita 58.4 kusini magharibi mwa Mji wa Morogoro, ni mahali ambapo kinapatikana kilele cha juu cha Mlima Uluguru kiitwacho Kimhandu (2,638m a.s.l). Ni eneo kubwa la Majani ya Montane na aina nyingi za Mimea ya kipekee pia ni chanzo cha Mito mingi ikiwa ni pamoja na Mito mikubwa kam Mito ya Ruvu na Mgeta.
Ili ufike Lukwangule kwa Gari ni umbali wa Km 6-10 kisha unaanza kupanda Safu za Milima Lukwangule kwa mwendo wa Saa 9 hadi kufikia Kilele sehemu ijulikanayo Kimhandu.
Njia nyingine ya kufika Lukwangule kutokea Morogoro Mjini kwa kutumia Gari kupitia mashariki mwa Milima maeneo ya Kiroka, Mkuyuni, Matombo, Mvuha hadi Kasanga Mission ambapo ndio mwisho wa Gari. Baada ya hapo utaanza kutembea hadi Kijiji cha Ukwama ambapo utalala katika Mahema. Asubuhi ya siku inayofuata utatumia masaa 3 kutembea hadi kileleni.
B. CHANGAMOTO ZILIZOPO
Vivutio vingi vilivyopo katika maeneo yaliyopo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Manispaa yana upungufu ufuatao; -
C: UTATUZI WA CHANGAMOTO HIZO
Jitihada zifanyike kuhakikisha changamoto tajwa zinafanyiwa kazi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa